MONUSCO yatahadharisha sintofahamu DRC

Kusikiliza /

Walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo DRC, wako katika tahadhari kubwa na tayari kutumia nguvu kuwalinda raia wa Goma dhidi ya mashambulizi ya kundi la waasi wa M23.

Kaimu mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC Moustapha Soumaré amezitaka pande zinazokinzana kusitisha mapigano akisema Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO, umesikitishwa na mapigano yaliyoibuka baada ya M23 kuwavamia jeshi la nchi hiyo mwishoni mwa wiki eneo liitwalo Mutaho lililoko kilometer kumi na nne Kaskazini Magharibi mwa Goma.

Kwa mujiobu wa MONUSCO silaha nzito ikiwamo mizinga ilitumika katika mashambulizi. Momusco imeonya kwamba jaribio lolote la kuingia Goma litachukuliwa kama tishio kwa raia.

Katika tamko lake Moustapha ametaka pande zote kuheshimu makubaliano ya amani, usalama na ushirikiano na kuruhusu mchakato wa kisiasa kuelekea amani uendelee.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031