Mmea wa quinoa unaweza kuchangia kutokomeza njaa: FAO

Kusikiliza /

Mmea wa quinoa unaweza kuchangia pakubwa katika kutokomeza njaa kwa sababu ya sifa zake za lishe na manufaa ya kiuchumi, limesema Shirika la Chakula na Kilimo, FAO. Katika muktadha huo, FAO imesema nchi za Argentina, Bolivia, Chile, Ecuador na Peru zipo katika nafasi nzuri zaidi ya kuendeleza ukuzaji wa quinoa, pamoja na thamani yake ya lishe na utamaduni.

Hata hivyo, wakulima wa quinoa sasa wanakabiliwa na changamoto, kwani kuna ongezeko la mahitaji ya quinoa kwenye masoko ya kimataifa, na hivyo kutoa nafasi ya mapato mbadala ya kiuchumi kwa wakazi wa maeneo kunakokuzwa quinoa.

Kutokana na utambuzi huo, FAO itatekeleza mkakati wenye fungu la michakato na hatua kwenye ngazi ya kikanda ili kuziwezesha nchi hizo kuitikia changamoto hiyo ya mahitaji makubwa ya quinoa kwa njia ya kina, na kuongeza uzalishaji endelevu wa quinoa na ulaji wake katika nchi linapozalishwa, ili kuimarisha mifumo ya chakula katika nchi hizo.

Mkakati huo wa usadizi wa kitaalam kwa uzalishaji endelevu wa quinoa katika kuongeza na kuimarisha mfumo wa chakula katika nchi za ukanda wa Andea, utaendeshwa kutoka kwa ofisi ya FAO Amerika ya Kusini, kama mwitikio kwa ombi la wizara za kilimo Argentina, Bolivia, Chile, Ecuador na Peru.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29