Mjumbe wa UM nchini Iraq ashutumu mashambulizi ya hivi majuzi mjini Baghdad

Kusikiliza /

Martin Kobler

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq ameshutumu vikali  misururu ya mashambulizi ya hivi majuzi na kutoa wito kwa pande zote kushirikiana  kwa pamoja katika kupata amani ukiwa ndio ujumbe wake wa mwisho anapoondoka tangu achukue wadhifa huo mwaka 2011.Kupitia ujumbe huo mashambulizi yalifanyika kwenye mji mkuu Baghdad karibu watu 30 waliripotiwa kuuawa kupitia misusuru ya mashambuliz kwa njia ya mabomu ya kutegwa ndani ya magari hiyo jana.

Mashambulizi hayo yalijiri baada ya siku nzima ya kufunga wakati waumini wa kislamu wanaposherekea mwezi mtukufu wa Ramadan. Martin Kobler ambaye pia ni mjumbe wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq amesema kuwa mashambulizi yanayowalenga waislamu walio misikitini ni uovu akiongeza kuwa mwezi mtukufu wa Ramadan ni wakati wa kusameheana wala si wakati ambapo mashambulizi yanaongezeka.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29