Matarajio yetu ni ulimwengu ambako kila mimba inatakiwa:UM

Kusikiliza /

Mama na mtoto

Siku ya Idadi ya Watu Duniani huadhimishwa kila mwaka mnamo tarehe 11 Julai. Mwaka huu, kauli mbiu ya siku hiyo ambayo imeadhimishwa wiki hii imekuwa: mimba miongoni mwa wasichana wadogo. Takriban wasichana milioni 16 chini ya umri wa miaka 18 hujifungua mamba kila mwaka, huku wengine milioni 3.2 wakitoa mimba kwa njia zisizo salama. Wengi wao, ambao ni asilimia 90 ya wasichana hao wanaoshika mamba katika nchi zinazoendelea, wameolewa. Lakini kwa wengi wao, mimba si kitu wanachochagua, bali zinatokana na ubaguzi, ukiukwaji wa haki zao, ukosefu wa elimu na dhuluma za kingono.Idadi ya watu duniani sasa ni zaidi ya bilioni saba, ikiwa imepanda kutoka bilioni mbili nukta tano mwaka 1950.

Kwa kuangazia mimba za wasichana wadogo, Umoja wa Mataifa una matarajio ya kuweka ulimwengu ambako kila mimba inatakiwa, kila uzazi ni salama na ndoto ya kila kijana inatimizwa. Kwa mengi zaidi, ungana na Jason Nyakundi kwa makala hii.

(Makala ya Jason Nyakundi)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031