Madawa hatari ya kuulia wadudu yasitishwe kwenye nchi zinazoendelea:FAO

Kusikiliza /

usmabazaji wa dawa

Shirika la chakula na kilimo FAO limesema madawa hatari ya kuulia wadudu imefika wakati yasitishwe katika nchi zinazoendelea . Ikitoa mfano FAO imesema tukio la Bihar India ambako watoto 23 wa shule wamefariki dunia kutokana na kula chakula shuleni kilichochanganyika na dawa ya monocrotophos, ni kumbusho muhimu la kuchapuza kuondoa madawa hayo hatari kutoka katika masoko kwenye nchi zinazoendelea. FAO inasema dawa ya Monocrotophos ni aina ya dawa ya kuulia wadudu ambayo FAO na shirika la afya duniani WHO inaichukulia kama dawa hatari sana.

Uzoefu katika nchi nyingi zinazoendelea unaonyesha kwamba usambazaji na matumizi ya dawa hatari kama hizo mara nyingi ni tishio kwa maisha na afya ya binadamu lakini pia ni hatari kwa mazingira.

FAO inasema tukio la Bihar pia linaonyesha umuhimu wa kuhifadhi dawa hizo palipo na usalama ili kuepuka athari kubwa kama vifo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930