ILO yataka sera za uundwaji zaidi nafasi za ajira nchi za G-20

Kusikiliza /

Wakati tatizo la ajira bado liko juu katika mataifa ya G-20, shirika la kazi duniani ILO limetoa wito wa kuwepo na sera za kuongeza wigo wa nafasi za ajira zinazojumuisha kila mmoja ili kufikia lengo la nchi hizo la kuwa na ukuaji uchumi imara, endelevu na wenye uwiano.Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa ILO Guy Ryder ana imani kuwa juhudi zaidi zinaweza kufanyika, kwani uzoefu unaonyesha kwamba kiwango cha juu cha upatikanaji ajira na ukuaji unaojumuisha wote vinawezekana kupitia sera madhubuti za kiuchumi, sera za ajira, za masoko ya kazi na za kulinda masuala ya kijamii ambazo zinataganya sawia faida za ukuaji wa uchumi.

Bwana Ryder ameyasema hayo kwenye mkutano na waandishi habari alipokuwa akiwasilisha takwimu mpya za mtazamo wa masoko ya ajira na changamoto kwa nchi za G-20.

Takwimu hizo zimeandaliwa na ILO na OECD kwa ajili ya mkutano wa mawaziri wa kazi na ajira kutoka nchi za G-20.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2015
T N T K J M P
« dis    
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
262728293031