Idadi ya watu wanaotumia madawa ya kufubaza nguvu za ukimwi imeongezeka-UM

Kusikiliza /

Zaidi ya watu milioni 10 wanaishi na virusi vya Ukimwi wameripotiwa kufikiwa na madawa yanayotumika kufubaza ukali wa virusi hivyo, ripoti ya Umoja wa Mataifa imesema na kuongeza kuwa hali hiyo ilishuhudiwa katika kipindi cha mwaka uliopita 2012.

Ripoti hiyo iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa pamoja baina ya shirika la afya ulimwenguni WHO, lile linalohusika na watoto UNICEF na lile linalohusika na ukimwi UNAIDS imesema kuwa idadi ya watu wanafikiw ana madawa hayo inaweza kuongezeka iwapo kutaaandaliwa mipango mizuri zaidi ya namna ya kuwafikia.

Kumekuwa na ongezeko la watu milioni 1.6 ikilinganishwa na ripoti ya mwaka wa nyuma 2011 kuelekea 2012.

Ripoti hiyo pia imetoa mwongozo unaowataka watu wanaishi na virusi vya ugonjwa huo kunaza kutumia dawa hizo mapema kadri iwezekanavyo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2017
T N T K J M P
« ago    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930