Hezbollah kujumishwa kwenye orodha ya makundi ya kigaidi hakutoathiri UNIFIL:UM

Kusikiliza /

Derek Plumbly

Mratibu maalumu wa Umoja wa mataifa kwa ajili ya Lebanon Derek Plumbly amesema uamuzi wa Muungano wa Ulaya wa kulijumuisha Hezbollah kama kundi la kigaidi haitoathiri mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL.Amesema Umoja wa Mataifa ni Umoja wa Mataifa ulioundwa na nchi zote na UNIFIL inajumuisha majeshi kutoka nchi zaidi ya 30. Hivyo anaamini kwamba kila mtu nchini Lebanon na katika ukanda mzima anafaidika na usalama na utulivu ambao unapatikana kutokana na kuwepo kwa vikosi vya UNIFIL Kusini mwa nchi hiyo.

 Bwana Plumby ameyasema hayo alipozungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wake na Rais wa zamani wa Lebanon Amine Gemayel, ambapo walijadili masuala yahusiyo kanda na Lebanon hususani upande wa ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa na Lebanon.

Masuala hayo yanajumuisha wakimbizi wa Syria na jinsi gani ya kuhakikisha msaada wanaouhitaji wanaupata lakini pia msaada kwa serikali yaLebanon,manispaa na jumuiya zinazohifadhi wakimbizi hao

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2014
T N T K J M P
« nov    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031