Heko Baraza kuu kwa kuridhia siku ya choo duniani: Eliasson

Kusikiliza /

Vyoo

Nafurahi ya kwamba nchi wanachama zimeridhia azimio la kutangaza rasmi tarehe 19 Novemba kuwa siku ya kimataifa ya choo duniani, ni kauli ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson aliyotoa punde baada ya kupitishwa kwa azimiohilomjiniNew Yorkhii leo. AmepongezaSingaporekwa kuchochea mpango huo na kusema kuwa utambuzi wa siku hiyo utaibua uelewa juu ya umuhimu wa binadamu kuwa na huduma ya choosafina salama wakati huu ambapo mtu mmoja kati ya watatu hana huduma ya choo. Naibu Katibu Mkuu amesema ukosefu wa choo umesababisha vifo vya watoto Elfu Mbili kila siku kutokana na magonjwa ya kipindupindu na kwamba kiuchumi hasara itokanayo na uchafu yafikia dola Bilioni Mia Mbili Sitini. Ameenda mbali na kusema haikubaliki ya kwamba wanawake wako hatarini kubakwa na kunyanyasa wakati wakisaka hudumu hiyo ambayo haitiliwi maanani. Ametaka kila nchi kuchochea harakati za kuboresha huduma hiyo ili kila mkazi wa dunia hii awezek kuipata kwa kuwa ni haki ya msingi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031