Hali ya usalama inatia shaka Sudan: UM

Kusikiliza /

UNAMID wafanya ziara kambi ya Kalma Darfur kusini, Sudan

Umoja wa Mataifa umeonya kwamba mapigano nchiniSudankati ya majeshi ya serikali na waasi yaliyosababisha vifo vya wafanyakazi wawili wa asasi za kiraia huko Darfur ni  ishara ya kudorora kwa usalama na kikwazo cha kufikisha misaada katika jimbohilolenye mizozo.

(TAARIFA YA GEORGE)

Mratibu wa shughuli za misaada ya kibinadamu nchini Sudan Ali Al-Za’tari,amelaani mauwaji hayo kwa kusema kuwa wafanyakazi hao wako Darfur kwa ajili ya kusaidia misaada ya kiutu hivyo kitendo cha kuwashambulia na kufifisha maisha yao hakikubaliki.

 Bwana  Al-Za’tari amesema kuwa Umoja wa Mataifa umeingiwa na simanzi  kutokana na kupoteza kwa watumishi wake waliokuwa wakifanya kazi na shirika la kimataifa la World Vision linaendesha shughuli za usamaria mwema.

Mapigano hayo baina ya vikosi vya serikali na makundi ya wanamgambo yamesababisha kujitokeza kwa hali ya sintofahamu.

Mfanyakazi mwingine wa shirikahiloameripotiwa kuwa katika hali mbaya na amekimbizwa hospitali kwa matatibabu.

Kauli ya kutaka kuwepo utulivu kwenye eneohiloiliyotolewa na Bwana Al-Za’tari inafuatia kauli nyingine kama hiyo iliyotolewa Mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu juu ya vikosi vya ulinzi wa amani Hervé Ladsous ambaye alitaka pande zinazozozana kuweka chini silaha.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2017
T N T K J M P
« jan    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728