Hakuna aliyekamatwa kufuatia shambulio dhidi ya askari wa Tanzania: Chambas

Kusikiliza /

Mohammed Ibn Chambas, Mkuu wa UNAMID

Mkuu wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika, huko Darfur, UNAMID, Mohammed Ibn Chambas amesema hadi sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kufuatia shambulio lililosababisha vifo vya walinda amani Saba wa Tanzania tarehe 13 mwezi huu huko Kusini mwa Darfur. Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani baada ya kulihutubia Baraza la Usalama, Bwana Chambas amesema kinachofanyika sasa ni uchunguzi utakaowezesha pia kuundwa kwa bodi ya uchunguzi na kwamba serikali ya Tanzania imeonyesha nia ya kushiriki uchunguzi huo.
"Tumejulishwa na mamlaka za Tanzania kuwa nayo pia imedhamiria   kutuma ujumbe kufanya kazi nasi pamoja na serikali ya Sudan katika uchunguzi, na pia serikali ya Sudan, gavana wa jimbo la Sudan Kusini na mwendesha mashtaka wa Darfur wamewasiliana nasi na kusema wako tayari kuchunguza."

Bwana Chambas amesema kinachotia moyo ni kwamba pande zote husika zimebaini kuwa shambuliohilolilikuwa la kikatili na hivyo ni vyema kubaini wahusika ili waweze kufikishwa mbele ya sheria.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031