Cousin kuzuru Mataifa manne barani Afrika:WFP

Kusikiliza /

Ertharin Cousin, WFP

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la chakula duniani Ertharin Cousin anatarajiwa kuanza safari yake ya siku kumi ya nchi nne Afrika kesho.Taarifa ya George Njogopa inafafanua.(RIPOTI YA GEORGE)

Ratiba ya safari yake inaonyesha ataanzia nchini Zimbabwe ambako atatembelea hospitali moja ambayo WFP inatoa huduma ikiwemo chakula kwa wagonjwa wa kifua kikuu na wale wenye vrusi vya ukimwi.

Baada ya hapo ataelekea nchini Afrika Kusin na kisha kuelekea  Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo nchi ambayo WFP inatoa msaada kwa watu zaidi ya milioni moja walioathiriwa na mapigano yanayoendelea.

Hatimaye atakamilisha safari yake kwa ziara fupi nchini Rwanda ambako pamoja na kukutana na wakimbizi wa Congo ambao WFP nawapa hisani, lakini pia atatembelea mradi wa nyumba kwa ajili ya watu walioko katika mazingira hatarishi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930