Ban azungumza na waziri wa mambo ya nje wa Misri kwa simu

Kusikiliza /

Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ban Ki-Moon, leo amefanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Mohammed Kamal Amr, na kuelezea kusikitishwa kwake na vifungo vinavyoendelezwa nchini humo na waranta za kuwakamata viongozi kundi la Muslim Brotherhood na wengineo.Bwana Ban amemkumbusha Waziri huyo wa Misri kuhusu majukumu ya Misri ya kimataifa na haja ya kuheshimu kikamilifu haki za uhuru wa kujumuika, kujieleza, na kupata haki kisheria.

Ameweka bayana kuwa kulipiza kisasi au kutenga chama chochote kile kikuu au jamii fulani nchini Misri hakuwezi kukubalika kamwe. Ametangaza tena uungaji wake mkono kwa watu wa Misri katika kutimiziwa matakwa yao, pamoja na kutoa wito yafanywe mazungumzo ya amani ambayo yanajumuisha matabaka yote kisiasa kwa ajili ya mustakabali wa taifa hilo.

Amesema Umoja wa Mataifa utaendelea kuunga mkono serikali ya Misri ambayo inawajibika kikamilifu kwa watu wa Misri.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031