Ban alaani vikali ongezeko la machafuko Misri

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amelaani vikali ongezeko la machafuko nchini Misri ambayo yamesababisha vifo vya makumi ya watu na mamia yaw engine kujeruhiwa, kufuatia maandamano mnamo Ijumaa na Jumamosi. Kwa mujibu wa taarifa ilotolewa na msemaji wake, Bwana Ban ametuma risala za rambi rambi kwa familia za wahanga na kuwatakia walojeruhiwa nafuu haraka.

Katibu Mkuu ametoa tena wito kwa mamlaka za mpito nchini humo kuchukuwa kikamilifu wajibu wa kudhibiti maandamano ya amani na kuhakikisha ulinzi wa raia wote wa Misri. Amevitaka vikosi vya usalama vya Misri kuheshimu haki za binadamu kikamilifu katika vitendo vyao, zikiwemo haki za kujieleza na kujumuika, huku akiwasihi waandamanaji kujiepusha na ghasia ili kuendeleza mwenendo wa amani wa maandamano yao.

Taarifa inasema Bwana Ban ametoa wito kwa raia wote wa Misri kushughulikia tofauti zao kwa njia ya mazungumzo, na kutoa wito kwa pande zote kujikita katika harakati jumuishi za maridhiano. Amesema kamwe ghasia haziwezi kuchukua nafasi ya suluhu la kisiasa na hivyo kutoa wito kwa viongozi wote wa Misri kutanguliza matakwa ya taifa lao mbele ya matakwa yao binafsi au vyama na siasa zao.

Bwana Ban amerejelea kusema Bwana Mohammed Morsi na viongozi wengine wa chama cha Muslim Brotherhood ambao sasa wapo kizuizini waachiliwe huru mara moja au kesi zao kuangaliwa kwa njia ya uwazi.

 
Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031