Ban akutana na waziri wa sheria wa Israel Bi Tzipi Livni:

Kusikiliza /

KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon leo amekuatana na waziri wa sheria wa Israel na mpatanishi mkuu wa mazungumzo ya amani baina ya Israel na Palestina Bi Tzipi Livni.

Katibu Mkuu ameelezea uungaji mkono wake wa kuanza tena majadiliano ili kufikia lengo la kuwa na suluhu ya mataifa mawili. Pia ameishukuru hatua ya ujasiri ya hivi karibuni iliyochukuliwa na waziri mkuu Benjamini Netanyahu kuhusu suala hili.

Ban amekaribisha ushiriki na mchango wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu wa kuwa na kamati ya ufuatiliaji wa amani. Amesisitiza umuhimu wa kuweka mazingira bora kwa ajili ya kuanza tena mazungumzona kuzichagiza pande zote kuchukua hatua zaidi kuhakikisha mafanikio ya suala hili.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2016
T N T K J M P
« ago    
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
2627282930