Nyumbani » 29/07/2013 Entries posted on “Julai 29th, 2013”

Baraza la Usalama lalaani shambulizi la bomu kwenye ubalozi wa Uturuki Mogadishu

Kusikiliza / Baraza la Usalama

    Wanachama wa Baraza la Usalama wamelaani vikali shambulizi la bomu la kujitoa mhanga kwenye jengo moja la ubalozi wa Uturuki mjini Mogadishu, Somalia, mnamo Julai 27, na ambalo lilisababisha kifo cha mtu mmoja na kuwajeruhi wengine kadhaa. Wanachama hao wa Baraza la Usalama wameelezea huzuni yao na kutuma risala za rambirambi kwa familia [...]

29/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban alaani vikali shambulizi kwenye jengo la Waturuki Somalia

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amelaani vikali shambulizi la kigaidi lililotekelezwa dhidi ya ofisi ilokaliwa na wafanyakazi wa kituruki mjini Mogadishu. Bwana Ban ametuma risala za rambirambi kwa serikali na watu wa Uturuki, na kwa watu wa Somalia. Katika taarifa ilotolewa na msemaji wake, Bwana Ban amesema Uturuki ni mshirika muhimu kwa [...]

29/07/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Shirika la la OzHarvest lashirikiana na UNEP kuwalisha watu 5000 mjini Sydney

Kusikiliza / ozharvest

Jinsi ambavyo wanadamu wanavyotumia chakula chao ni ishara kuwa watu katika Karne hii ya 21 si waangalifu na hawafanyi jitihada za kukilinda huku karibu theluthi moja ya chakula kinachozalishwa kikitupwa. Kwa mara ya kwanza kabisa nchini Australia OzHarvest kama mshirika mkuu wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP nchini Australia lililo kwenye kampeni [...]

29/07/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban atiwa wasiwasi na kuzorota hali ya usalama Iraq

Kusikiliza / Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ameelezea hofu yake kuhusu kuzorota kwa hali ya usalama nchiniIraq, na kulaani vikali vitendo vya kigaidi na ghasia za kidini ambazo zinalenga kusambaratisha mfumo wa kijamii wa nchi hiyo. Amesema ripoti za mauaji ya watu wapatao 50 hii leo katika mashambulizi ya mabomu ya magari kwenye maeneo [...]

29/07/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mtaalam wa UM akaribisha kuachiwa huru kwa wafungwa, huku akielezea hofu yake kufuatia wanaokamatwa

Kusikiliza / Tomás Ojea Quintana

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadam nchini Myanmar, Tomás Ojea Quintana, amekaribisha hatua ya msamaha wa rais wa nchi hiyo Julai 23 ambapo watu  73  walofungwa kwa kuwa na dhana tofauti  huku akielezea wasiwasi kufuatia kukamatwa kwa wanaharakati (TAARIFA YA GEORGE)  Kuachiwa kwa wafungwa hao kumeelezewa na mtaalamu wa Umoja [...]

29/07/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Maandalizi ya uchaguzi Mali yalikuwa mazuri licha ya changamoto Kaskazini: Afisa UM

Kusikiliza / Mpigaji kura, Mali

Wakati wananchi wa Mali wamehitimisha mchakato wa upigaji kura kwenye uchaguzi wa Rais, Naibu Mkurugenzi kutoka kitengo cha usaidizi wa upigaji kura cha Umoja wa Mataifa Ali Diabacté amesema zoezi hilo limefanyika kwa amani na maandalizi yalikuwa mazuri licha ya kwamba waliojitokeza kupiga kura walikuwa ni wengi maeneo ya Kusini mwa Mali kuliko Kaskazini.Bwana Diabacte [...]

29/07/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Elimu kuhusu jinsia na huduma za afya kujadiliwa na wataalamu Botswana

Kusikiliza / Watoto darasani

Wataalamu na watunga sera kutoka Mashariki na Kusini mwa Afrika watakutana mjini Gaborone, Botswana, Julai 30 na 31, ili kutathimini matokeo ya ripoti mpya kuhusu matatizo yanayowakabili vigori na vijana kuhusiana na afya na elimu ya jinsia.Mkutano huo ambao umeitishwa na shirika la Umoja wa mataifa la masuala ya ukimwi UNAIDS na lile la elimu, [...]

29/07/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Watu wenye matatizo ya ugonjwa wa ini wana haki ya kupata huduma bora za matibabu

Kusikiliza / Mtu apokea chanjo

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na madawa ya kulevya na uhalifu ametoa wito wa kuongeza juhudi ili kuzalisha mbinu na mikakati ya kukabiliana na tatizo la ugonjwa wa ini huku akitaka kutolewa kwa matibabu sawa kwa mamia ya watu wanaathiriwa na matumizi ya madawa ya kulevya.Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya [...]

29/07/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNFPA kuandaa maonyesho juu ya ndoa za utotoni

Kusikiliza / Ndoa za utotoni,picha ya Stephanie Sinclair

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na idadi ya watu linatazamia kuratibu maonyesho ya wazi yatayotanyika Washington kueleza namna vitendo vya kuwaozesha watoto wa kike ambao hawajafikia umri wa kuolewa.UNFPA inasema kuwa kila mwaka zaidi ya wasichana 39,000 wenye umri wa chini ya miaka 18 huolewa jambo ambalo imesema kuwa ni uvunjifu wa haki za [...]

29/07/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa UM awataka viongozi wa kisiasa Iraq kukomesha machafuko:

Kusikiliza / Machafuko,Iraq

Afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa mataifa nchini Iraq ameelezea hofu yake kufuatia wimbi jipya la milipuko ya mabomu yaliyotegwa kwenye gari lilozuka Jumatatu na kusababisha vifo vya watu kadhaa na kujeruhi wengine.Afisa huyo ambaye ni kaimu mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq bwana Gyorgy Busztin amesema kinachomtoa mashaka makubwa ni [...]

29/07/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kambi ya Za'atari yazidi kukumbwa na changamoto:UNICEF

Kusikiliza / Watoto katika kambi ya Za'atari

Hii leo ni mwaka mmoja tangu kufunguliwa kwa kambi ya Za'atari nchini Jordan inayohifadhi wakimbizi wa Syria, ikiwa na wakimbizi Laki Moja na Ishirini, huku zaidi ya nusu wakiwa ni watoto. Marc Vergara afisa uhusiano kutoka UNICEF anazungumzia hali ilivyo kwenye kambi hiyo ambayo sasa ni ya pili kwa ukubwa duniani. (SAUTI YA MARC)

29/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

MONUSCO yalaani ukatili unaofanywa na kikundi cha m23

Kusikiliza / Wapignaji wa M23

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC umeelezea wasiwasi wake juu ya madai ya kwamba kikundi cha waasi cha M23 kinahusika na mauji, utumikishaji wa lazima wa raia kwenye kikundi hicho na hata kukamata raia. Taarifa ya Jason Nyakundi inafafanua zaidi. (Taarifa ya Jason) Kufuatia hali hiyo Gavana wa jimbo [...]

29/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban akutana na waziri wa sheria wa Israel Bi Tzipi Livni:

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon leo amekuatana na waziri wa sheria wa Israel na mpatanishi mkuu wa mazungumzo ya amani baina ya Israel na Palestina Bi Tzipi Livni. Katibu Mkuu ameelezea uungaji mkono wake wa kuanza tena majadiliano ili kufikia lengo la kuwa na suluhu ya mataifa mawili. Pia ameishukuru hatua ya [...]

29/07/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kuendelea kukariri uhalifu unaoendelea Syria bila vitendo hakutoshi: Pinheiro

Kusikiliza / Paulo Pinheiro

pinhMkuu wa Tume huru ya kimataifa ya kuchunguza madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Syria, Paulo Pinheiro, ameliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuwa kuendelea kukariri vitendo vya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nchini Syria bila kufanya lolote hakutoshi, huku akitoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua. Joshua Mmali anayo [...]

29/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban amezungumza na makamu wa Rais wa muda wa Misri:

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezungumza kwa njia ya simu na makamu wa Rais wa mpito wa Misri Mohamed ElBaradei. Ban amemwelezea hofu yake kuhusu mwelekeo wa serikali ya mpito. Amelaani vikali machafuko nchini humo ambayo yamepoteza maisha ya watu wengi. Ban ameitolewa wito serikali hiyo ya mpito kuchukua majukumu ya kuhakikisha [...]

29/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya wakimbizi Elfu 10 wa Ivory coast waondoshwa Liberia

Kusikiliza / Wakimbizi wa Ivory Coast

Shirika la kuhudumia wakimbizi wa Umoja wa Mataifa, UNHCR linasema kuwa zaidi ya raia Elfu Kumi wa Ivory Coast waliokimbilia Liberia miaka miwili iliyopita kutokana na ghasia za baada ya uchaguzi wamerejea nyumbani mwaka huu. Assumpta Massoi na taarifa kamili.(TAARIFA ASSUMPTA) Wakimbizi hao wengi wao walikuwa wakiishi kwenye kambi na kaya za wenyeji huko Grand [...]

29/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNFPA yajikita kupambana na ukeketaji Uganda

Kusikiliza / Watoto wa kike

Baada ya shirika la afya duniani , WHO, kutoa ripoti inayoonyesha hali ya ukeketaji barani Afrika na Mashariki ya mbali katika ukanda wa Afrika Mashariki Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa idadi ya watu UNFPA unaendelea na juhudi za kuelimisha jamii juu ya namna ya kuepuka kitendo hicho haramu. Akiongea kutoka nchini Uganda Afisa wa [...]

29/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930