Nyumbani » 25/07/2013 Entries posted on “Julai 25th, 2013”

Ukaguzi wa Umoja wa Mataifa umeimarisha stadi za wakaguzi kutoka Tanzania: Uttouh

Kusikiliza / Ludovik Uttouh na Assumpta Massoi

Mapema wiki hii wajumbe wa bodi ya ukaguzi wa Umoja wa Mataifa walikutana mjini New York Marekani ambapo pamoja na mambo mengine walitia saini ripoti za ukaguzi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa mwaka wa fedha 2012. miongoni mwa wajumbe hao ni Ludovick Uttouh, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali yaTanzania. Katika [...]

25/07/2013 | Jamii: Mahojiano, Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Pillay alaani vikali mauaji ya kiongozi wa upinzani nchini Tunisian

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amelaani vikali mauaji ya leo Alhamisi ya mwanasiasa wa upinzani nchini Tunisia na kuwataka watu wan chi hiyo na wanasiasa kuungana kupinga majaribio ya kusambaratisha mchakato wa kipindi cha mpito cha kidemokrasia nchini humo. Mohamed Brahmi, mbunge, alipigwa risasi na kuuawa nje ya [...]

25/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ujumbe wa UM ulioenda Syria wahimitisha ziara: Ban

Kusikiliza / Ban Ki-moon na John Kerry

   Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon leo amekuwa na mazungumzo na Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani, John Kerry kwenye makao makuu ya umoja huo mjini New York, ambapo amesema timu aliyoituma Syria kufanya mazunguzo na serikali imehitimisha kazi yake leo na atapatiwa taarifa kuhusu ziara hiyo baadaye. Bwana Ban amesema [...]

25/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mpango wa kuikwamua Somalia kutoka kwenye hali ya sasa wazinduliwa

Kusikiliza / Hassan-Sheikh Mohamoud

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamoud amesema kuwa nchi yake imekaribisha mpango mpya kutoka kwa mataifa yaliyoathiriwa zaidi ya mizozo ya g7+ wa kuikwamua nchi hiyo kutoka kwenye hali iliyopo sasa. Rais Hassan Sheikh Mohamoud ameyasema haya  alipokwa akitoa hotuba kwenye mkutano kuhusu mipango ya kisiasa ya hadi mwaka 2016 mjini Mogadishu.Mkutano huo uliwashirikisha maafisa [...]

25/07/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Pillay aitaka Israel kutupilia mbali sheria inayolenga kuhamisha watu wa jamii ya Bedoui

Kusikiliza / Navi Pillay

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay  ameitaka serikali ya Israel kuufanyia mabadiliko msuada wa sheria ambao ikiwa utatekelezwa utasababisha kubomolewa kwa hadi vijiji 35 kwenye jangwa la Negev na kutwaliwa kwa ardhi ambapo huenda watu 30,000 hadi 40,000 kutoka jamii ya Bedouin wakatimuliwa kutoka kwa ardhi ya mababu zao. Jason [...]

25/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mafuriko Mashariki mwa DPRK yaacha wengi bila makazi.

Kusikiliza / Mafuriko, DPRK

Mvua kubwa za msimu huko Jamhuri ya kidemokrasia ya watu waKorea, DPRK zilizonyesha wiki mbili zilizopita zimesababisha mafuriko kwenye maeneo mengi nchini humo hususan maeneo ya kaskazini na kusini mwa mji mkuu Pyongyangna mamia hawana makazi. Ripoti ya Alice Kariuki inafafanua zaidi. (TAARIFA YA ALICE KARIUKI) Kumekuwa na taarifa zinazopishana kuhusiana na idadi ya watu waliojeruhiwa [...]

25/07/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa wamaliza malipo ya fidia kwa Kuwait

Kusikiliza / UM

Tume ya kulipa fidia ya Umoja wa Mataifa imeipatia Kuwait zaidi ya dola Bilioni Moja ikiwa ni kiasi kilichokuwa kimebakia cha madai yake kufuatia uvamizi uliofanywa naIraq. George Njogopa anaripoti (RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA) Hadi sasa kamishna hii tayari imeshatoa fidia kiasi cha dola za Marekani billion 42.3 ambazo ni kati ya dola bilioni 52.4 zilizotengwa [...]

25/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hezbollah kujumishwa kwenye orodha ya makundi ya kigaidi hakutoathiri UNIFIL:UM

Kusikiliza / Derek Plumbly

Mratibu maalumu wa Umoja wa mataifa kwa ajili ya Lebanon Derek Plumbly amesema uamuzi wa Muungano wa Ulaya wa kulijumuisha Hezbollah kama kundi la kigaidi haitoathiri mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL.Amesema Umoja wa Mataifa ni Umoja wa Mataifa ulioundwa na nchi zote na UNIFIL inajumuisha majeshi kutoka nchi zaidi ya 30. Hivyo [...]

25/07/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Amani DRC na nchi za maziwa makuu yaangaziwa

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linakutana leo kujadili mustakabali wa amani katika ukanda wa nchi za maziwa makuu na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.Taarifa zaidi na Flora Nducha (SAUTI YA FLORA NDUCHA) Mkutano huo wa leo unakuja takribani miezi mitano baada ya kusainiwa kwa mkataba wa amani, usalama na ushirikiano ambapo mkutano [...]

25/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ripoti za ukaguzi wa mahesabu ya Umoja wa Mataifa zatiwa saini

Kusikiliza / UN flags

Bodi ya ukaguzi ya Umoja wa Mataifa imeridhia na kutia saini ripoti 15 za ukaguzi wa mahesabu ya Umoja wa Mataifa kwa mwaka wa fedha 2012. Hatua hiyo imefanyika wakati wa kikao cha bodi hiyo mjini New York, Marekani kinachojumuisha wadhibiti na wakaguzi wakuu wa mahesabu ya serikali kutoka Tanzania, Uingereza na China ambazo ndio [...]

25/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031