Nyumbani » 22/07/2013 Entries posted on “Julai 22nd, 2013”

Yalopita si ndwele, tugange yajayo: Rais Kikwete

Kusikiliza / Wanajeshi waagwa , Tanzania

Nchini Tanzania walinzi amani Saba waliouawa kwenye shambulio la kuvizia hukoDarfur, Sudan tarehe 13 mwezi huu wameagwa katika shughuli ya kitaifa ya maombolezo.Amiri jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, Rais Jakaya Kikwete aliongoza shughuli hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya waombolezaji wakiwemo wawakilishi kutoka Umoja wa Mataifa, serikali ya Tanzania na mabalozi bila kusahau [...]

22/07/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Uungwaji mkono ukeketaji watoto wa kike na wanawake wapungua: UNICEF

Kusikiliza / fgm

Idadi kubwa ya wakazi wa nchi ambako ukeketaji wanawake na watoto wa kike hufanyika wanapinga kuendelea kufanyika kwa kitendo hicho na hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF iliyotolewa Jumatatu. Flora Nducha na maelezo zaidi. (RIPOTI YA FLORA NDUCHA) Matokeo ya ripoti hiyo yanatokana na [...]

22/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Licha ya shambulio kamwe hatutarudi nyuma: Rais Kikwete

Kusikiliza / Rais na Bi Kikwete wakitoa heshima ya mwisho mbele ya majeneza yenye miili ya askari

Nchini Tanzania hii leo imefanyika shughuli ya kitaifa ya kuaga miili ya askari saba wa kitanzania waliouawa kwenye shambulio huko Darfur nchini Sudan tarehe 13 mwezi huu. Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete aliongoza mamia ya waombolezaji kwenye shughuli hiyo iliyofanyika jijini Dar Es salaam huku akiwasihi walinda amani wa Tanzania kamwe wasirudi nyuma na wakati [...]

22/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lajadili hali ya kisiasa Burundi

Kusikiliza / Onanga-Anyanga

TAARIFA YA JOSHUA MMALI Bwana Onanga-Anyanga, ambaye ni Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi, BNUB, ameliambia Baraza la Usalama kuwa ili kuandaa uchaguzi wa amani, uwazi na haki, mazungumzo yanatakiwa yafanyike kuhusu kuweka mazingira bora kwa ajili ya uchaguzi mwaka 2015. Bwana Anyanga amesema serikali na [...]

22/07/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Hatua nzuri zimepigwa na FAO: Ripoti ya DFID:

Kusikiliza / fao_logo_web

Shirika la chakula na kilimo FAO limepiga hatua katika miaka miwili iliyopita lakini bado kuna mengi ya kufanya, kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa na kuchapishwa na idara ya Uingereza ya maendeleo ya kimataifa DFID. Alice Kariuki na taarifa zaidi. (RIPOTI YA ALICE KARIUKI) Ripoti hiyo kuhusu FAO imekuja kukiwa kumepita miaka miwili tangu taaisi [...]

22/07/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa WFP asifu juhudi za maendeleo vijijini nchini Rwanda

Kusikiliza / Ertharin Cousin

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, Ertharin Cousin, leo amehitimisha ziara ya siku tatu nchini Rwanda, ambayo imekuwa kituo cha mwisho cha ziara yake barani Afrika, ambayo iliangazia masuluhu ya vijijini kwa matatizo ya njaa na utapiamlo. Akiwa nchini Rwanda, Bi Cousin amekutana ana kwa ana na watu ambao wamekuwa wakipokea [...]

22/07/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mabadiliko ya sheria kuhusu haki maeneo ya kazi yaanza kutekelezwa nchini Bangladesh

Kusikiliza / ILO_logo

Mabadiliko kwenye sheria ya kazi ya mwaka 2006 nchini Bangladesh iliyoanza kutekelezwa tarehe 15 mwezi huu ni moja wapo ya sehemu ya kutimiszwa kwa ahadi ya serikali ya kuheshimu haki ya uhuru wa kushauriana na kushughulia zaidi masula ya usalama kazini na afya. Jason Nyakundi na taarifa zaidi. (RIPOTI YA JASON NYAKUNDI) Mabadiliko hayo yaliyofanywa [...]

22/07/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa UM nchini Iraq ashutumu mashambulizi ya hivi majuzi mjini Baghdad

Kusikiliza / Martin Kobler

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq ameshutumu vikali  misururu ya mashambulizi ya hivi majuzi na kutoa wito kwa pande zote kushirikiana  kwa pamoja katika kupata amani ukiwa ndio ujumbe wake wa mwisho anapoondoka tangu achukue wadhifa huo mwaka 2011.Kupitia ujumbe huo mashambulizi yalifanyika kwenye mji mkuu Baghdad karibu watu 30 waliripotiwa kuuawa kupitia misusuru [...]

22/07/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Maradhi ya moyo yasalia kuwa muuaji namba moja:WHO

Kusikiliza / Maradhi yasiyoambukizwa

  Shirika la afya duniani WHO limesema maradhi ya moyo yanasalia kuwa chanzo namba moja cha vifo duniani ikiwa ni moja ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza.Maradhi hayo yamekatili maisha ya watu karibu milioni 17 mwaka 2011 ikiwa ni sawa na watu 3 kati ya kila vifo 10. WHO inasema watu milioni 7 katiyaohufa na maradhi [...]

22/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Matatizo ya chakula na utapia mlo yaendelea kuisakama Malawi:UM

Kusikiliza / Malawi yaendelea kukumbwa na matatizo ya chakula

Sera za karibuni za Malawi kuhusu usalama wa chakula zimeshindwa kuliondoa taifa hilo kwenye tatizo sugu la ukosefu wa chakula na utapia mlo kwa mujibu wa mtalaamu huru wa haki za binadamu na haki ya chakula wa Umoja wa Mataifa. Grace Kaneiya na taarifa zaidi (RIPOTI YA GRACE KANEIYA) Zaidi ya asilimia 50 ya wananchi wa [...]

22/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa DRC nchini Tanzania kupatiwa vyandarua kujikinga na Malaria

Kusikiliza / Kambi ya Nyarugusu

Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na chama cha msalaba mwekundu nchini Tanzania umepanga kusambaza vyandarua kadhaa kwa  wakimbizi kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC waliko katika kambi ya Nyarugusu Mkoani Kigoma, kaskazini mwaTanzania. Mpango huo ambao pia unaungwa mkono na chama cha kimataifa cha msalaba mwekundu umelenga kukabiliana na tatizo la Malaria ambalo linatakwa [...]

22/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031