Nyumbani » 19/07/2013 Entries posted on “Julai 19th, 2013”

Serikali ziheshimu haki ya watu ya faragha: Mtaalam wa UM

Kusikiliza / Frank La Rue

Uwezo wa serikali kufuatilia mienendo ya watu umewezesha kuingilia maisha ya watu binafsi, ambao huenda hata wasijue ikiwa wanatizamwa, au kuweza kupinga uvamizi kama huo dhidi ya maisha yao binafsi faraghani. Hayo yamesemwa na mtaalam maalum wa haki ya kujieleza katika Umoja wa Mataifa, Frank La Rue katika ripoti yake ya hivi karibuni zaidi, akisisitiza [...]

19/07/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wananchi wa Burundi wamuenzi Mandela kwa msaada wake

Kusikiliza / mandela

Mnamo tarehe 18 Julai wiki hii, ulimwengu mzima uliadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mandela, ili kumuenzi Nelson Mandela, rais wa zamani wa Afrika Kusini na Shujaa wa kupigania uhuru na haki za binadamu. Hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, ilifanyika hafla maalum ya kuadhimisha siku hiyo kwenye ukumbi wa mikutano ya Baraza Kuu, [...]

19/07/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na ripoti za mapigano ya kikabila Guinea

Kusikiliza / Informal Thematic Debate of the 66th Session of the General Assembly on “The Road to Rio+20 and beyond”

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ameelezea kusikitishwa na ripoti za mapigano ya kikabila kusini mwa Guinea, ambayo yamesababisha vifo vingi na watu kupoteza mali zao. Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wake, Bwana Ban ametoa wito wa utulivu na kuwataka watu wa Guinea kujiepusha na vitendo vyote ambavyo huenda vikazorotesha amani na [...]

19/07/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mashambulizi dhidi ya walinda amani yanaweza kuwa ni uhalifu wa vita:ICC

Kusikiliza / Fatou Bensouda

Mwendesha mashitaka kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC Fatou Bensouda amelaani mauaji ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania na kujeruhi wengine 17 wakiwemo wanajeshi na polisi wanaouunda kikosi cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika UNAMID. Watu hao waliuawa tarehe 13 Julai huko Kusini mwa Darfur Sudan [...]

19/07/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban akaribisha kurithiwa sheria ya utaratibu wa uchaguzi Afghanistan

Kusikiliza / Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekaribisha hatua ya rais wa Afghanistan kurithia sheria inayodhibiti mifumo na wajibu wa taasisi za kusimamia uchaguzi nchini humo.Bwana Ban amesema sheria hiyo ni hatua muhimu katika kuweka utaratibu thabiti wa uchaguzi wa urais na mabaraza ya mikoa, ambao utafanyika mnamo April 5 mwakani. Kwa mujibu wa [...]

19/07/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Swala la utekelezaji wa haki za watu wenye ulemavu laangaziwa

Kusikiliza / Ulemavu

Mkutano unaongazia haki za watu wenye ulemavu ulioanza juzi unakamilika leo hapa Umoja wa Mataifa mjini New York. Mkutano huo ambao ni maandalizi ya mkutano mkuu wakati baraza  kuu la UM  litakapokutana mwezi september mwaka  huu pamoja na mambo mengine umegusia namna nchi wanachama wanavyotekeleza wajibu wao kuhusu haki ya kundi hilo. Ungana na Joseph [...]

19/07/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya haki za binadamu inafuatilia hali Guinea

Kusikiliza / Ofisi ya haki za binadamu

Ofisi ya Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa imesema hali ya utulivu inaonekana imerejea inafuatilia nchini Guinea baada ya siku tatu za ghasia za kikabila, kati ya kabila la Guerze na Konianke kwenye kata ya Koule, kwa karibu kilomita 45 kutoka mji wa Nzerekore, ambazo zilianza mnamo Julai 15. Mapigano hayo yanadaiwa kuzuka kutokana [...]

19/07/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mbinu mpya zahitajika katika utunzi wa sera za uwekezaji: UNCTAD

Kusikiliza / unctad_logo_copy1-300x257

Kamati ya biashara na maendeleo katika Umoja wa Mataifa, UNCTAD imetoa mwelekeo mpya wa uwekezaji dunani wenye lengo la kuhakikisha hatua zozote za uwekezaji zinachochea ukuaji uchumi jumuishi na maendeleo endelevu. Mwongozo huo upo katika muhtasari wa toleo kuhusu makubaliano mapya ya kimataifa kuhusu uwekezaji uliokuwa umeandaliwa kwa ajili ya semina ya uwekezaji iliyofanyika Finland ambapo [...]

19/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yafanya jitihada za kuwasiadia wakimbizi kutoka DRC walio nchini Uganda

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka DRC nchini Uganda

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linafanya jitihada za kuwapelekea mahitaji muhimu wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DRC. Wakimbizi hao walianza kukimbia makwao tarehe 11 mwezi Julai baada ya uvamizi uliofanywa kweneye eneo la Kamango mashariki mwa DRC. Jason Nyakundi anaripoti.  (Taarifa ya Jason) UNHCR inasema kuwa juma moja baada [...]

19/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO yawapiga jeki wakulima wadogo wadogo Lebanon

Kusikiliza / Wakulima, Lebanon

Kwa miaka mingi Lebanon imekuwa ikiagiza chakula toka nje kwa ajili ya kutosheleza mahitaji ya watu wake lakini kutokana na mpango huo wa FAO huenda hali hiyo ikapungua. Sekta ya kilimo inatajwa kuwa ndiyo uti wa mgongo wa taifa hilo ambalo wananchi wake wengi wanategemea kujiingizia kipato. Utafiti mmoja ulioendeshwa na FAO hivi karibuni katika [...]

19/07/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Twahitaji taarifa kuhusu viongozi wa Misri waliotiwa nguvuni: Pillay

Kusikiliza / Navi Pillay

Ofisi ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema wiki moja tangu kuiandikia waraka serikali ya mpito ya Misri ikitaka kufahamu misingi ya kisheria iliyosababishwa Rais wa zamani wa nchi hiyo Mohammed Morsi na maafisa wengine waandamizi wa serikali kuendelea kuwa nguvuni hakuna jibu lolote kutoka serikali hiyo ya mpito. Taarifa zaidi na Assumpta [...]

19/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Rasimu ya sheria ya vyombo vya habari Somalia iangaliwe upya: UM

Kusikiliza / Rupert Colville

Ofisi ya Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu imetaka kupitiwa upya kwa rasimu inayohusu sheria ya vyombo vya habari nchini Somalia.  George Njogopa na maelezo Zaidi:  (Taarifa ya George)  Ofisi hiyo ya Umoja wa Mataifa imeitaka mamlaka ya Somalia kuangalia upya rasimu hiyo ili iweze kwenda sawia na viwango vya haki za binadamu.  [...]

19/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yabaini hatari za kiafya zinazokabili makundi ya wahamiaji wanaoelekea Kusini mwa Afrika

Kusikiliza / IOM

Matokeo ya awali ya utafiti mpya uliofanywa na shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM kwa ubia na taasisi ya masuala ya afya Kusini na mashariki mwa Afrika, PHAMESA) yanaonyesha hatari za kiafya zinazowakabili raia wanaohama makwao kutoka nchi za Maziwa makuu, Afrika Mashariki na hata pembe ya Afrika kuelekea Kusini mwa Afrika. Matokeo hayo yamewasilishwa [...]

19/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031