Nyumbani » 18/07/2013 Entries posted on “Julai 18th, 2013”

Amani imeimarika Côte d'Ivoire, sheria zitekelezwe: UM

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limekutana kujadili hali ya amani nchiniCôte d'Ivoire aambapo wajumbe wa baraza hilowameelezwa kwamba licha ya hatua kubwa ya usalama iliyopigwa na taifa hilo ambalo lilikumbwa na mzozo baada ya uchaguzi mkuu, hatua zaidi za utekelezaji wa haki za binadamu zinahitajika Akiongea na waandishi wa habari baada ya [...]

18/07/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UM kusaidia kutokomeza kipindupindu Haiti

Kusikiliza / Valerie Amos

Mratibu wa Misaada ya Dharura wa Umoja wa Mataifa Valerie Amos ametangaza mgao wa ziada wa dola za Marekani1.5 kutoka Mfuko wa Dharura (Cerf) ili kukabiliana na kipindupindu nchini Haiti. fedha za nyongeza ziinakuja wakati muhimu, ambapo wagonjwa wa kipindupindu wanatarajiwa kuongezeka kwa ajili ya msimu wa mvua. Ugonjwa huu umepelekea watu 8100 kupoteza maisha [...]

18/07/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Watoto wakumbwa na madhila ya vita: UM

Kusikiliza / Leila Zerrougui

Mwakilshi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto na athari za kivita Leila Zerrougui amekamilisha ziara yake nchini Syria , Jordan, Iraq, Turkey, na Lebanon ambako ameshuhudia madhara ya mgogoro wa Syria kwa watoto waliko nchini humo na katika ukanda huo kwa ujumla. Akitoa tathimini ya ziara hiyo Bi Zerrougu amesema amekutana [...]

18/07/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Duru nyingine ya mabadiliko yahitajika kwa Uchina kuendelea kufanikiwaIMF:

Kusikiliza / imf-logo_high

Uchumi wa Uchina unatarajiwa kukua kwa asilimia 7 na robo tatu kwa mwaka huu , ikiwa ni sawa na kiwango cha mwaka jana lakini hatari kidogo imejitokeza wamesema wachumi wa shirika la fedha duniani IMF. Katika ripoti yao kuhusu uchumi wa China wachumi hao wamesisitiza umuhimu wa mabadiliko ili kupata walaji zaidi na ukuaji endelevukatika [...]

18/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICC yakataa ombi la Libya la kusitisha kujisalimisha kwa Saif Al-Islam Gaddafi :

Kusikiliza / Saif Al-Islam Gaddaffi

Kitengo cha rufaa cha mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC Alhamisi kimekataa ombi la uongozi wa Libya la kutaka kumsalimisha kwa mahakama hiyo Saif Al-Islam Gaddaffi na kukumbusha kwamba Libya ina wajibu wa kumsalimisha bwana Gadaffi kwenye mahakama hiyo. Serikali ya Libya iliwasilisha ombi Juni 7 mwaka huu ikitaka kusitishwa kumsalimisha mshukiwa wakati uamuzi [...]

18/07/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mandela amwagiwa sifa na viongozi Afrika

Kusikiliza / Nelson Mandela

Katika kuadhimisha Siku hii ya Kimataifa ya Mandela, viongozi mbali mbali wa zamani kutoka Afrika wamekuwa wakielezea sifa za Mandela wakikumbuka mchango wake katika maisha ya mwanadamu. Miongoni mwao ni Rais mstaafu wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi(CLIP MWINYI) Mwingine aliyemtolea Nelson Mandela sifa kem kem ni Dk. Salim Ahmed Salim, ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu [...]

18/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya Kimataifa ya Mandela

Kusikiliza / Nelson Mandela akizungumza - Baraza Kuu la UM

Leo ni Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela, shujaa wa kupigania uhuru Afrika Kusini na mpiganiaji haki za binadamu, ambaye leo ikiwa siku ya kuzaliwa kwake, amehitimisha miaka 95. Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeadhimisha siku hii kwa kuangalia video fupi ya Mandela, akiongea nyakati tofauti, ukiwemo mwaka 1990, alipotoa hotuba kwenye Umoja wa [...]

18/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wafanyakazi wa UM wamuenzi Mandela kwa kuwasaidia waathirika wa Sandy

Kusikiliza / Wafanyi kazi wa UM

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya Mandela Umoja wa Mataifa unaungana na wito wa wakfu wa Mandela wa kutaka watu "kuchukua hatua na kuchagiza mabadiliko" wito ambao unawataka watu kujitolea kwa dakika 67 ili kuwasaidia wengine katika sehemu mbalimbali ikiwemo hospital, kufundisha watoto, kugawa chakula kwa wasio na makazi ,au shughuli yoyote ya huduma kwa [...]

18/07/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban ashutumu dhuluma zinazoendeshwa na jeshi la DRC dhidi ya wanamgambo wa M23

Kusikiliza / Waasi wa M23

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amesikitishwa na ripoti kuhusu kudhulumiwa kwa wafungwa wa kundi la M23 na pia ripoti za kuchomwa kwa miili ya wanangambo hao vitendo vinavyondeshwa na wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC MONUSCO umelitilia maanani zaidi suala hili ukilitaka jeshi [...]

18/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNRWA na EU washirikiana katika elimu kwenye dharura:

Kusikiliza / watoto wa shule-UNRWA

Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limekuwa likifanya kazi kutoa msaada wa elimu na kisaikolojia kwa watoto wa wakimbizi wengi wa Kipalestina ambao wametawanywa na machafuko Syria. Sasa UNRWA inapigwa jeki na Muungano wa Ulaya katika suala hili. George Njogopa na taarifa kamili (TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA) Msaada kutoka [...]

18/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya Mandela ni wakati wa kuchukua hatua na kuyakumbuka aliyotenda:Ban

Kusikiliza / Siku ya Mandela Julai 18

Watu duniani kote wanachagizwa kuchukua hatua kwa niaba ya wengine Alhamisi ya leo katika kusherehekea siku ya kimataifa ya Nelson Mandela. Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa MAtaifa Ban Ki-moon ambaye anaadhimisha siku hii kwa kukumbuka maisha na mchango mkubwa wa kiongozi huyo wa kimataifa ambaye kwa sasa bado yuko mahututi hospitali. [...]

18/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031