Nyumbani » 11/07/2013 Entries posted on “Julai 11th, 2013”

Baraza la Usalama laongeza muda wa ujumbe wa UNMISS

Kusikiliza / Walinda amani wa UNMISS

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limeptisha azimio la kuongeza muda wa kuhudumu kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS kwa kipindi cha mwaka mmoja, hadi Julai 15, 2014. Baraza hilo limesema hali nchini Sudan Kusini inatishia amani na usalama wa kimataifa katika ukanda mzima. Baraza hilo pia limesema jukumu la [...]

11/07/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Serikali zisisahau kuchagiza sekta binafsi zinapoondoa vizuizi vya kibiashara: UNCTAD

Kusikiliza / Ripoti hiyo ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika 2013

Serikali za Afrika zinafanya kampeni kubwa ya kupunguza vizuizi vya kibiashara baina ya nchi barani humo, lakini wakati zikifanya hivyo, zinapaswa zichukuwe hatua mathubuti kuzipa msukumo sekta za kibinafsi. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya Kamati ya Biashara na Maendeleo katika Umoja wa Mataifa, UNCTAD, ambayo imeonya kuwa nchi za Afrika zisipotoa msukumo [...]

11/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Leo ni siku ya idadi ya watu duniani

Kusikiliza / Felister Bwana

Dunia ikiwa inaadhimisha siku ya idadi ya watu leo huku ujumbe wa maadhimisho hayo kwa mwaka huu ukiwa ni kutokomeza mimba za mapema , mfuko wa Umoja wa Mataifa wa idadi ya watu UNFPA ndiyo wenye dhamana ya kuhakikisha ujumbe huo unawafikia walengwa na kutekelezwa kikamilifu. Nchini Tanzania UNFPA kwa kushirikiana na wadau wanatoa elimu [...]

11/07/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ban azungumza na waziri wa mambo ya nje wa Misri kwa simu

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ban Ki-Moon, leo amefanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Mohammed Kamal Amr, na kuelezea kusikitishwa kwake na vifungo vinavyoendelezwa nchini humo na waranta za kuwakamata viongozi kundi la Muslim Brotherhood na wengineo.Bwana Ban amemkumbusha Waziri huyo wa Misri kuhusu majukumu ya Misri ya kimataifa na [...]

11/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa waizuru kambi ya Ein El-Hilweh nchini Lebanon

Kusikiliza / Robert Watkins

Mratibu wa masuala ya kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa Robert Watkins ameitembelea kambi ya Ein El-Hilweh iliyo kusini mwa Lebanon hii leo akiandamana na mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto kweye mizozo Bi Leila Zerrougui pamoja na mkurugezi wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA nchini [...]

11/07/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lakutana kuhusu Sudan na Sudan Kusini

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo wanafanya mikutano kuhusu nchi za Sudan na Sudan Kusini. Kikao cha Baraza hilo cha asubuhi kwa saa za New York kimefanywa faraghani, lakini baadaye kitafanyika kikao cha wazi, ambako ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu Sudan Kusini itawasilishwa.Kikao cha mchana pia kitaangazia Jamhuri ya Kidemokrasi ya [...]

11/07/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Msajili wa ICC aeleza kwa nini wameshindwa kumkamata Rais Bashir wa Sudan:

Kusikiliza / Herman Von Hebel

Msajili wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC iliyoko The Hague nchini Uholanzi ametababaisha tofauti ya utendaji kati yake na mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama hiyo. Bwana Herman Von Hebel akizungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa amefafanua masuala kadhaa ikiwemo suala la kushindwa kumkamata Rais wa Sudan Al-Bashir (SAUTI YA HERMAN HEBEL) Na [...]

11/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wakubali mwaliko wa Syria kukamilisha uchunguzi

Kusikiliza / Katibu Mkuu akutana na mkuu wa UM kuhusu matumizi ya kemikali Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekutana na profesa Åke Sellström, mkuu wa ujumbe wa Umoja wa mataifa wa kuchunguza madai ya matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria.Profesa Sellström amemweleza Ban hatua zilizofikiwa  ambazo ni pamoja na kuzichambua kwa kina taarifa walizopewa na nchi wanachama na shughuli za uchunguzinkatika nchi jirani. Mwakilishi [...]

11/07/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kiwango cha uzalisahi nafaka kuongezeka mwaka 2013-FAO

Kusikiliza / Mazao ya nafaka kuimarika mwaka 2013:FAO

Kiwango cha uzalishaji wa nafaka duniani kinatazamia kuweka historia ya aina yake duniani katika msimu wa mwaka 2013, wakati hali ikiwa hivyo hali ya ukosefu wa chakula inatazamiwa kuwa mbaya zaidi nchini Syria, Afrika ya Kati na Afrika Magharibi.(Taarifa zaidi na George Njogopa) Uzalishaji wa nafaka unakadiriwa kukua kwa wastani wa asilimia 7 katika kipindi [...]

11/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tuwekeze kwa wasichana wabadili jamii: Ban

Kusikiliza / womenundp-300x257

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amezungumza katika siku ya idadi ya watu duniani na kusema ikiwa jamii itajitoa na kuwekeza raslimali za elimu ,afya na ustawi wa wasichana, kundi hilo litakuwa kichocheo kikuu kwa ajili ya mabadiliko chanya katika jamii. Katika taarifa yake hiyo Ban amesema kuwa kufanya hivyo kutaleta mabadiliko [...]

11/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nusu ya watoto wanaoacha shule wanaishi katika maeneo yaliyoathirika na migogoro:UNESCO

Kusikiliza / Watoto wa shuile DRC

Waraka uliotolewa na utafiti wa kimataifa wa shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO unaonyesha kwamba nusu ya watoto milioni 57 ambao wameacha shule wanaishi katika nchi zilizoathirika na vita. Alice Kariuki anaripoti (TAARIFA YA ALICE KARIUKI) Ripoti hiyo iliyotolewa kwa ushirikiano na shirika la Save the children inaadhimisha miaka 16 [...]

11/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031