Nyumbani » 09/07/2013 Entries posted on “Julai 9th, 2013”

Ban akutana na wawakilishi wa Bolivia, Cuba, Ecuador, Nicaragua na Venezuela

Kusikiliza / Ban Ki-moon

Katibu Mkuu amesisitiza kuwa anaelewa hofu ilotokana na tukio hilo la kusikitisha, na kusema kwamba alifurahia kuwa halikusababisha madhara yoyote kwa usalama wa rais Morales na ujumbe wake. Ameongeza kuwa ni muhimu kuzuia kutokea kwa matukio kama hayo siku zijazo. Bwana Ban amesema kiongozi wa taifa na ndege yake hawapaswi kuhatarishwa. Ameelezea matumaini yake kuwa [...]

09/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM walaani mlipuko uliotokea katika viunga vya Kusini mwa Beirut :

Kusikiliza / Lebanon

Viongozi wa Lebanon na vyama vya siasa lazima waungane kupinga vitisho hivyo kwa usalama wa nchi9 yao, utulivu na kujitahidi kurejesha jukumu la taasisi za Lebanon. Mratibu huyo anatumai kwamba tukio la leo litachunguzwa kwa kina na wahusika kufikishwa kwenye vyombo vya sheria haraka iwezekanavyo

09/07/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa UM awatakia Wasomali wote Ramadhan njema:Kay

Kusikiliza / Nicholas Kay

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Bwana Nicholas Kay, amewatakia Wasomali wote heri ya mwezi mtukufu wa mfungo wa Ramadhan.Wakati Wasomali wakiungana na Waislamu wote kote duniani kwa mfungo wa Ramadhan Kay amesema huu ni mwezi wa kiroho na kutafakari , na ni wakati mzuri wa kutimiza mambo mengi yanayohitaji kufanyika ili kudumisha [...]

09/07/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu lajadili mchango wa Umoja wa Mataifa katika uongozi wa kimataifa

Kusikiliza / Baraza Kuu

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo limefanya mdahalo kuhusu azimio linalohusu mchango wa Umoja wa Mataifa katika uongozi wa kimataifa na pia kujadilia utekelezaji wa matokeo ya mkutano wa Rio+20 kuhusu maendeleo endelevu. Joshua Mmali amefuatilia mkutano wa leo TAARIFA YA JOSHUA Baraza hilo Kuu limeanza kikao chake kwa kutoa heshima kwa marehemu Stoyan [...]

09/07/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban aitaka Syria kumaliza machafuko wakati wa Ramadhan

Kusikiliza / Machafuko Syria

Wakati waisalamu kote duniani wakiwa wameanza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amelitaka taifa la Syria ambalo limekuwa katika mapigano kwa muda mrefu kuupatia suluhu ya kisaisa mzozo huo. Akitoa wito wake kuhusu mfungo huo Ban amesema ni muhimu kuwafikia wahitaji wa vyakula , maji na [...]

09/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Machafuko yanatishia usalama Misri: UM

Kusikiliza / Navi Pillay

Ofisi ya haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa umeelezea kusikitishwa kwake na kuendelea kwa machafuko nchini Misri kunakofuatia kuondolewa kwa serikali ya kundi la Muslim brotherhood. George Njogopa anasimulia zaidi.  Kiasi cha watu 90 wameuwawa tangu kuzuka kwa machafuko hayo ya kisiasa hapo July 3, huku idadi waliojeruhiwa ikifikia zaidi ya 1,3000.  Kamishna wa [...]

09/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ashutumu mauaji na ghasia zinazoendela Misri

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon ameelezea masikitiko yake kutokana  ghasia zinazoendelea nchini Misri wakati mzozo wa kisiasa unapoendela.Ban anasema kuwa anasumbiliwa na ripoti za kuuawa kwa zaidi ya watu 50 hii leo. Katibu mkuu ametuma rambi rambi zake kwa familia za wale waliouawa. Alice Kariki anaeleza zaidi. (RIPOTI YA ALICE KARIUKI) [...]

09/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNHCR azuru Moghadishu katika mkesha wa ramadhan na kuonyesha mshikamano:

Kusikiliza / Antonio Guterres

  Kamishina mkuu wa wakimbizi wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezuru Somalia Jumanne na kuonyesha uungaji mkono wake wa mchakato wa amani unaoendelea katika taifa hilo lililosambaratishwa na vita kwa zaidi ya miongo miwili. Ziara yake ilipangwa ili kwenda sambamba na mkesha wa mfungo wa Ramadhan ili kuoshesha mshikamano wake kwa watu waSomaliakutokana na [...]

09/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mradi wa kuwashirikisha raia wa Sudan Kusini walio nje kwenye masuala ya afya wazinduliwa na IOM

Kusikiliza / IOM

Huku taifa la Sudan likiadhimisha mwaka wa pili wa kuwa huru, Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limezindua mpango wenye lengo la kuboresha huduma kwa wanadamu hususan zile za kiafya kwa kuwashirikisha wataalamu raia wa Sudan Kusini walio kwenye mataifa ya kigeni.Mradi huo unaofadhiliwa kwa kima cha dola 200,000 kutoka mfuko wa maendeleo wa IOM [...]

09/07/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji wa Ethiopa waliokwama Yemen wamerejea nyumbani:IOM

Kusikiliza / Jumbe Omari Jumbe

  Kundi la watu 131 wahamiaji kutoka Ethiopia ambao walikwama nchini Yemen sasa wamefanikiwa kurejea nyumbani kwa hiari kwa usafiri wa ndege ya shirika la kimataifa linalohusika na uhamiaji IOM. Kuwasili kwa raia hao mjini Addis Ababa, kunafanya idadi jumla waliokwisha rejea nyumbani kufikia 765 tangu lilipoanza zoezi hilo Juni mwaka huu. Zoezi la kuwarejesha [...]

09/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930