Nyumbani » 08/07/2013 Entries posted on “Julai 8th, 2013”

Nafasi sawa na utajiri unaowanufaisha wote ni muhimu kwa maendeleo endelevu: Ban

Kusikiliza / Usawa wa kijinsia ni muhimu:Ban

Malengo ya maendeleo ya milenia yamepata ufanisi mkubwa katika kuchagiza hatua za kimataifa kuhusu masuala kadhaa, lakini, bado tofauti za kijamii na kiuchumi zinaendelea kukua katika nchi nyingi, ziwe maskini au tajiri, na hivyo kuweka doa la aibu kwa ahadi ya kimsingi ya mkataba mkuu wa Umoja wa Mataifa.Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ban Ki-Moon, [...]

08/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban amemteua Aboulaye Bathil wa Senegal kuwa naibu mwakilishi Mali:

Kusikiliza / MINUSMA

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametangaza uteuzi wa Adulate Bathily wa Senegal kuwa naibu mwakilishi wake maalumu wa mpango wa Umoja wa mataifa nchini Mali MINUSMA.Bwana Bathily amekuwa akifanya kazi kama waziri katika ofisi ya Rais nchiniSenegaltangu mwaka 2012.  Mwaka 1998 hadi 2001 alikuwa mbunge  kabla ya kushika wadhifa wa naibu spika [...]

08/07/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Papa Francis awaombea wahamiaji na wakimbizi kwenye kisiwa cha Lampedusa

Kusikiliza / Papa Franci azungumza na wakimbizi kutoka Afrika

  Papa Francis, kiongozi wa Kanisa Katoliki ametoa wito kuwepo uelewa na kuungana kwa ajili ya maelfu ya watu ambao huhatarisha maisha yao kila mwaka wakijaribu kuvuka bahari kwenda Uropa na kuwaombea wale ambao wamepoteza maisha yao wakijaribu kufanya hivyo. Papa Francis amesema hayo wakati wa ziara yake kwenye kisiwa cha Lampedusa, Italia leo Jumatatu.Saa [...]

08/07/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ni vyema Syria yataka kuzungumzia uchunguzi kuhusu silaha za kemikali: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amekaribisha kutaka kwa serikali ya Syria kuendelea na mazungumzo kuhusu ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuchunguza madai ya matumizi ya silaha za kemikali nchini humo.Kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa na msemaji wake, Bwana Ban ameelezewa kusikitishwa sana na madai hayo ya matumizi ya silaha za [...]

08/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kiswahili chaenziwa Washington DC

Kusikiliza / Rais mstaafu,Ali Hasani Mwinyi

Mwishoni mwa wiki jamii ya watu wanaozungumza Kiswahili wakiongozwa na jumuiya ya Watanzania waishioWashingtonDCna maeneo ya jirani, walishuhudia tamasha la utamaduni wa Kiswahili ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais mstaafu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hasani Mwinyi.Ungana na Joseph Msami katika makala ifuatayo itakayokujuza kilichojiri katika tamasha hilo.  

08/07/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ban atuma rambi rambi zake kutokana na ajali ya ndege iliyotokea jimbo la Carlifonia nchini Marekani

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon ameelezea huzuni yake baada ya ajali ya ndege ya shirika la Asiana iliyotokea kwenye eneo la San Fracisco jimbo la California nchini Marekani mwishoni mwa juma.Ban ametuma rambi rambi zake kwa familia zilizowapoteza wapendwa wao za wale waliojeruhiwa na wengine walioathiriwa na ajali hiyo kwa njia [...]

08/07/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mashindano ya 24 ya Tennis ya vijana kufanyika kwa msaada wa UNESCO

Kusikiliza / Mashindano ya 24 ya tennis kufanyika

Mashindano ya 24 ya vijana ya mchezo wa tennis , yajulikanayo kama BNP-Baribas Cup safari hii yanafanyika chini ya mwamvuli wa shirika la Umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO.Mashandinando hayo yatawaleta pamoja wachezaji kutoka kila pembe ya dunia kuanzia leo tarehe 8 Julai hadi tarehe 14 Juali mwaka huu karibu na mji [...]

08/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali Sudan Kusini yamulikwa kwenye Baraza la Usalama

Kusikiliza / Wakati wa  kikao kilichomulika Sudan Kusiini

Hapa mjini New York, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana leo kwa ajili ya Sudan Kusini, wakati taifahilolinapojiandaa kuadhimisha miaka miwili tangu kujipatia uhuru wake hapo kesho. Joshua Mmali amekuwa akifuatilia(TAARIFA YA JOSHUA) Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini ambaye pia ni mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini [...]

08/07/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Hali ya usalama inatia shaka Sudan: UM

Kusikiliza / UNAMID wafanya ziara kambi ya Kalma Darfur kusini, Sudan

Umoja wa Mataifa umeonya kwamba mapigano nchiniSudankati ya majeshi ya serikali na waasi yaliyosababisha vifo vya wafanyakazi wawili wa asasi za kiraia huko Darfur ni  ishara ya kudorora kwa usalama na kikwazo cha kufikisha misaada katika jimbohilolenye mizozo. (TAARIFA YA GEORGE) Mratibu wa shughuli za misaada ya kibinadamu nchini Sudan Ali Al-Za’tari,amelaani mauwaji hayo kwa [...]

08/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNSOM alaani mauaji ya mwandishi Gaalkacyo:

Kusikiliza / Nicholas Kay

Mwakilishi maalumu wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Nicholas Kay, amebaini kwa masikitiko makubwa mauaji ya Libaan Abdullahi Farah 'Qaran' ripota wa Kisomali wa Kalsan TV iliyoko mjini Gaalkacyo.Ripoti zinasema Libaan alipigwa risasi na kuuawa Jumapili usiki akirejea nyumbani kutoka kazini. Bwana Kay amesema huyu ni mwandishi wa tano kuuawa kwa mwaka [...]

08/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF yalaani mauaji ya watoto Nigeria

Kusikiliza / Shule iliyovamiwa na

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limelaani mauaji ya watoto nchini Nigeria ambapo trakwimu zinaonyesha kwamba tangu June 16 mwaka huu idadi ya watoto 48 na walimu 7 wameuwawa katika mashambulizi manne yaliyoripotiwa katika jimbo la Kaskazini. Mkurugenzi wa UNICEF kanda ya Magharibi na Kati mwa Afrika Manuel Fontaine pamoja na kutoa [...]

08/07/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali nchini Misri bado ni tete

Kusikiliza / Hali bado ni tete Misri

Taarifa kutoka nchini Misri zinasema takriban watu 42 wameuawa kwa kupigwa risasi mjini Cairo nje ya kambi ya kijeshi ambapo wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsy walikua wamekusanyika na wakiamini kuwa Rais wao anashikiliwa mahali hapo, Watu wengine 300 wamejeruhiwa. Kundi la Muslim  Brotherhood limewataka raia wa Misri kuwapinga wale wote linaowaita waporaji wa [...]

08/07/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mustakabali wa lugha ya Kiswahili unaridhisha:Mwinyi

Kusikiliza / Rais mstaafu wa Tanzania Al Hasani Mwinyi na Joseph Msami wa Idhaa hii

Wiki chache baada ya ripoti ya maendeleo ya binadamu ya shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP kuzindiliwa kwa Kiswahili, Rais mstaafu wa Tanzania Al Hasani Mwinyi amesema lugha hiyo sasa inakuwa kimataifa na kutaka vyombo vya habari kuisambaza maradufu. Taarifa zaidi na Grece Kaneiya Katika mahojiano maalum na idhaa ya Kiswahili [...]

08/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wapongeza ziara ya kiongozi wa Kurdistan nchini Iraq

Kusikiliza / Ramana ya Iraq

Mwana diplomasia wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq amepongeza tukio la ziara ya kiongozi wa Kurdish Masoud Barzani,aliyezuru Baghdad kwa maelezo kuu kitendo hicho kinafungua ukurasa mpya wa kiasiasa na hivyo kuweka mwanga wa kuwa na majadiliano ya mezani kwa ajili ya kusaka suluhu ya mikwamo inayojitokeza katika eneo hilo.Martin Kobler,ambaye ni mwakilishi maalumu wa [...]

08/07/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031