Zerrougui azuru Syria kunusuru watoto.

Kusikiliza /

Leila Zerrougui

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto na migogoro ya silaha Bi . Leila Zerrougui anatarajiwa kuzuru nchini Syria na nchi jirani kutathimini madhara kwa watoto kutokana na mgogoro nchini humo.

Bi Zerrougui ambaye anatarajiwa kuwasili nchini humo leo kadhalika atazitembela Uturuki na Lebanon ambapo atakutana na familia na watoto walioathiriwa na mapigano nchini Syria.

Mwakilishi huyo maalum wa Katibu wa Umoja wa Mataifa pia atatembelea operesehni za kibinadamu na kukutana na maafisa wa serikali, Umoja wa Mataifa na asasi za kiraia.

Katika ziara yake Bi Zerrougui ataainisha mahitaji na kuchochea utetezi juu ya ulinzi wa watoto walioathirika katika mgogoro huo na kuimarisha uwezo wa kusimamia na kutoa taarifa juu ya uhalifu mkuu unaofanywa dhidi ya watoto nchini Syria ili kuhakikisha washukiwa wa uhalifu huo wanawajibishwa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031