Watekelezaji wa ukatili wa kingono sasa kukiona cha mtema kuni: UM

Kusikiliza /

Kikao cha Baraza la Usalama la UM

Hatimaye Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limechukua hatua thabiti kuhakikisha kuwa watekelezaji wote wa vitendo vya ukatili wa kingono kwenye maeneo ya mizozo wanakumbana na mkono wa sheria. Na hii imekuja baada ya barazahilokupitisha azimio jipya ambamo kwalo linaimarisha juhudi za kuepusha watuhumiwa kukwepa mkono wa sheria wanapofanya vitendo hivyo siyo tu kwa wanawake na watoto wa kike bali pia wanaume na watoto wa kiume. Wajumbe kwa kauli moja wamepitisha azimio 2106 ambalo pamoja na kutambua kuwa ukatili wa kingono ni tishio la amani na usalama duniani, bali pia linataka uchunguzi wa kina wa uhalifu huo wa kingono na watuhumiwa kufunguliwa mashtaka kama njia mojawapo ya kuepusha vitendo hivyo. Azimio la leo linatia nguvu maazimio ya awali ya barazahilo, namba 1820, 1888 na 1960 ambayo yalielezea kuwa ukatili wa kingono unatumiwakamasilaha ya kivita kujenga hofu raia.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2017
T N T K J M P
« jan    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728