Utapiamlo waigharimu Ethiopia asilimia 16.5 ya pato lake la kitaifa

Kusikiliza /

Mtoto mwenye utapiamlo Ethiopia akichukuliwa vipimo

Taifa la Ethiopia linapoteza karibu asilimia 16.5 ya pato lake la kitaifa kutokana na athari za muda zinazotokana na utapiamlo miongoni mwa watoto kwa mujibu wa Shirika la mpango wa chakula duniani WFP. Hii ni moja ya takwimu zinazochipuza kutokana na utafiti wenye kichwa "Gharama ya Njaa barani Afrika" kuonyesha athari za utapiamlo kwenye mataifa 12 tofauti huku taifa la Ethiopia likiwa la tatu matokeo yake kuchapishwa. Kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita Ethiopia imepiga hatua muhimu  katika kupunguza njaa na utapiamlo. Huduma za kutoa lishe zinazolenga akina mama na watoto na miradi mingine ya kuboresha kilimo vimeziacha familia nyingi na afya bora na katika hali nzuri ya kujilisha. Shirika la WFP linasema kuwa athari zinazotokana na utapiamlo ni gharama kubwa kwa uchumi wa Ethiopia. Ripoti hiyo inakadiria kuwa utapiamlo unaigharimu Ethiopia mabilioni ya dola kila mwaka.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031