UNESCO yaeleza wasiwasi wa uharibifu wa maeneo ya kihistoria Syria

Kusikiliza /

Irina Bokova, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO

Wakati ripoti za kuharibiwa kwa maeneo kadhaa ya kihistoria na kidini nchini Syria zikiendelea kutolewa, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO limetaka maeneo hayo kulindwa dhidi ya mashambulizi yanayoendelea. Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova kwa kauli yake amesema ana wasiwasi mkubwa juu ya hatma ya maeneo hayo ya kihistoria na ametaka wahusika kuacha mara moja uharibifu wa maeneo hayo na badala yake wayaheshimu kwani ni ya kiimani na pia utamaduni wa raia wote wa Syria.

Amesema tofauti za kidini ambazo kwa miongo kadhaa zimekuwa moja ya hazina kubwa ya Syria nwa kwamba ulinzi na uhifadhi wa maeneo hayo kama vile maeneo ya kuabudu, maeneo ya kihistoria ambayo yana ubinifu wa kipekee wa majengo ni jambo linalogusa sana UNESCO.

Bi. Bokova amesema UNESCO iko tayari kupeleka wataalamu wake kutathmini kiwango cha uharibifu na kuandaa mikakati ya uhifadhi kadi hali ya usalama itakavyoruhusu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031