Ujerumani yaipa WFP euro milioni 15 kusaidia wakimbizi wa Syria:

Kusikiliza /

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP limepokea mchango wa Euro milioni 15 sawa na dola milioni 20 kutoka kwa serikali ya Ujerumani ambazo zitachangia msaada wa chakula kwa maelfu ya wakimbizi wa Syria ambao wamekimbia machafuko nchini mwao. Mchango huo wa karibuni unafanya jumla ya msaada uliotolewa na Ujerumani kwa WFP kusaidia operesheni za msaada Syria kufikia Euro milioni 25 sawa na dola milioni 33. Waziri wa ushirikiano wa uchumi na maendeleo wa shirikisho la Ujerumani Dirk Niebel ametangaza msaada huo mpya wa kwa WFP Jumapili wakati wa ziara yake kwenye kambi mbili zilizopo Nizip Kusini mwa Uturuki ambazo zinahifadhi wakimbizi wa Syria na kujionea hali halisi inayowakabili wakimbizi 15,000 wengi wao kutoka Aleppo na Kaskazini mwa Syria

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2017
T N T K J M P
« dis    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031