Silaha za kemikali huenda zimetumika Syria: Tume ya UM

Kusikiliza /

Paul Pinheiro

Tume iloteuliwa na Umoja wa Mataifa kufanya uchunguzi kuhusu Syria imesema kuna ushahidi mwinginr unaoonyesha kuwa silaha za kemikali zimetumika kwa viwango vidogo katika mgogoro unaoendelea nchini humo. George Njogopa anaripoti:

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

 Tume hiyo imesema kuwa imekusanya ushahidi wa kutosha kutoka kwa watu mbalimbali ikiwemo mashuhuda, wakimbizi na maafisa wa afya ambao wadhibitisha juu ya matumizi ya silaha za kemikali licha kwamba imekuwa ni vigumu kubainika mara moja aina ya kemikali hizo.

Katika ripoti yake iliyowasilishwa kwa Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, kamishna hiyo imesema kuwa mzozo waSyriaumefikia pahala ambako utu wa binadamu hauthaminiwi tena na kwamba vitendo vya unyama vimeendelea kukithiri, vikiwafanywa na pande zote mbili serikali na kundi la waasi.

Tume hiyo pia imesema kuwa pande zote zinazozozana zimeweka vizuizi ili kubinya huduma za utoaji misaada ya kibinadamu kwa mamia ya raia wanaoendelea kutabika sehemu mbalimbali ambao wengi wao hawana hudumakamaumeme, vyakula madawa na maji.

Bwana  Paulo Pinheiro ni Mwenyekiti wa Kamishna hiyo. 

 (SAUTI YA PAUL PINHEIRO)

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29