Tuyalinde mabahari, asema Ban kwenye Siku ya mabahari duniani

Kusikiliza /

Katika kuadhimisha Siku ya Mabahari Duniani, leo Juni 8, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, ametoa wito wa ushirikiano wa kuweka mawimbi mapya ya hatua za kuhakikisha mabahari endelevu kwa ajili ya watu na sayari dunia.  

Bwana Ban amesema, kuanzia biashara hadi chakula na kudhibiti tabianchi, mabahari ni sehemu muhimu ya uhai wa mwanadamu, hususan ule wa watu wanaoishi pwani, ambao mapato na utamaduni wao umeambatana kwa karibu sana na bahari.

Katibu Mkuu amesema ikiwa tunataka kunufaika kikamilifu kutokana na mabahari, ni lazima kuhakikisha ulinzi wa mazingira ya majini kutokana na uharibifu utokanao na kutupa kemikali, taka na uvuvi wa kupindukia.

Ametoa wito kwa mataifa yote kujitolea kwa hili, ikiwemo utekelezaji wa mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu sheria ya bahari.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031