Ripoti mpya yaonyesha ukuaji wa uwekezaji wa kigeni katika nchi maskini

Kusikiliza /

Ripoti iliyotolewa, UNCTAD

Ripoti mpya ya uwekezaji duniani mwaka 2013 inaonyesha kuwa uwekezaji wa moja kwa moja uliofanywa na wawekezaji wa kigeni katika nchi maskini, (FDI) uliongezeka kwa asilimia 20 mwaka 2012, na kufikia rekodi mpya ya dola bilioni 26.Ripoti hiyo ya kila mwaka ya uwekezaji uitwao Greenfield Investment, na ambayo imetolewa na Kamati ya Biashara na Maendeleo katika Umoja wa Mataifa, UNCTAD inaonyesha kuwa wingi wa uwekezaji huo ulifanywa na wawekezaji kutoka nchi zinazoendelea, zikiongozwa na India.

Uwekezaji huu ni katika nyanja mpya na unatofautiana na ule wa kampuni mpya kuungana na kampuni zilizopo tayari nchini au kununua kampuni zilizopo.

Ripoti hiyo iitwayo Mtandao wa thamani duniani: uwekezaji na biashara kwa maendeleo, imetolewa leo, na kuonyesha kuwa ukuaji huu katika viwango vya uwekezaji wa kigeni ulikuwa mkubwa zaidi nchini Cambodia (kwa asilimia 73), Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (asilimia 96), Liberia (asilimia 167), Mauritania (asilimia 105), Musumbiji (asilimia 105) na Uganda (asilimia 93).

Hata hivyo, nchi 20 maskini zilionyesha kushuka kwa viwango vya uwekezaji wa kigeni, zikiwemo Angola, Burundi, Mali na Visiwa vya Sulemani.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031