Noeleen Heyzer sasa kuwa mshauri maalumu wa UM Timor-leste:

Kusikiliza /

Noeleen Heyzer

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametangaza kuwa amemteua Bi. Noeleen Heyzer raia wa Singapore ambaye kwa sasa ni katibu mkuu wa tume ya uchumi na jamii kwa mataifa ya Asia na Pacific kuwa mshauri wake maalumu kwa ajili ya Timor-Leste. Pamoja na majukumu hayo mapya Bi. Hayzer ataendelea kuwa katibu mkuu wa ESCAP na hivyo kuvaa kofia mbili. Atakuwa akifanya kazi kwa karibu na serikali na mratibu mkazi wa Umoja wa mataifa Timor-Leste pia na na timu nzia iliopo nchini humo katika kuelekea ujenzi wa amani, ujenzi wa taifa unaojumuisha wote na maendeleo endelevu. Na kwa kuvaa kofia hiyo mpya pia Bi. Heyzer atachangia katika kuimarisha zaidi ushirikiano uliopo baina ya serikali ya Timor-Leste na Umoja wa Mataifa, hali ambayo itasaidia kuboresha zaidi ushirikiano wa kikanda na kuinua hali ya maisha ya watu katika taifa hilo

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29