Nchi 38 zatimiza lengo la kuangamzia njaa kabla ya ukomo uliowekwa:FAO

Kusikiliza /

mahindi barani Afrika

Jumla ya nchi 38 zimetimiza malengo ya kimataifa ya kupambana na njaa kabla ya muda uliowekwa 2015 kwa mujibu wa Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO. Mkurugenzi mkuu wa FAO José Graziano da Silva anasema kuwa mataifa hayo ni ishara kuwa kujitolea kisiasa , uongozi mwema na ushirikinao  inakuwa ni rahisi kuafikiwa kwa malengo ya kuangamiza njaa. Graziano da Silva amezitaka nchi zote kuwa na moyo huo  wenye malengo la kuangamiza njaa kwa kuzingati lengo la kuifanya njaa kuwa sufuri kufuatia uzinduzi uliofanywa na  katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon mwaka 2012. Nchi hizo Nchi hizo zikiwemo Algeria, Angola, Djibouti na Ghana zinatarajiwa kutuzwa kwenye mkutano wa juu katika makao makuu ya shirika la FAO tarehe 16 mwezi huu wakati kutakapoandaliwa mkutano wa juma zima.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031