Mtanzania kuongoza kikosi cha UNAMID, Darfur

Luteni Jenerali Paul Mella, Kamanda mpya wa kikosi cha UNAMID, Darfur

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon na Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini-Zuma wamemteua Luteni Jenerali Paul Ignace Mella kutokaTanzaniakuongoza kikosi cha pamoja cha kulinda amani cha taasisi hizo mbili hukoDarfur, UNAMID.  Luteni Jenerali Meela anachukua nafasi ya Mnyarwanda Luteni Jenerali Patrick Nyamvumba ofRwandaaliyemaliza muda wake mwezi Machi mwaka huu ambapo Bwana Ban amemshukuru kwa utendaji wake wa kujitolea wakati wa huduma hiyo.  Mkuu mpya wa kikosi cha UNAMID Luteni Jenerali Mella ana uzoefu mkubwa ndani ya jeshi laTanzaniaambapo hivi karibuni alikuwa mkuu wa intelijensia ya ulinzi na ameshawahi kushika nyadhifa zingine ikiwemo Mkuu wa masuala ya intelijensia ya kigeni ndani ya jeshi la wananchi waTanzania, TPDF. Kitaaluma, Luteni Jenerali Mella ana shahada ya uzamili katika masuala ya ulinzi na mikakati kutoka Chuo cha Taifa cha ulinzi Afrika Kusini.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031