Mtaalamu wa UM aitaka Nigeria kusitisha unyongaji

Kusikiliza /

Mauaji

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa dhidi ya mauji ya kiholela na unyongaji bwana Christof Heyns amelaani vikali unyongaji wa watu wane unaodaiwa kufanyika Juni 24 kwenye jimbo la Edo huko Nigeria. George Njogopa na taarifa kamili.

 (RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

 Bwana Heyns pia ametoa mwito wa kusitishwa utekelezaji wa adhabu ya kunyongwa inayowasubiri watu wengine 15 ambao wameendelea kusalia katika hali ya kihoro kikubwa.

Kabla ya kutekelezwa kwa adhabu ya safari hii, mara ya mwisho tukio la kunyongwa nchini Nigeria linalipotiwa kutokea mwaka 2006.

Mtaalamu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa anaingia na wasiasi kuhusiana na utekelezwaji wa adhabu hiyo kwani kunamazingira yanaasha maswali mengi kuhusiana na kuheshimiwa kwa sheria ya kimataifa inayohimiza uzingatiaji wa azimo la Umoja wa Mataifa juu ya haki ya kirai na haki ya kisiasa. Lakini pia ameitolea pia mwito serikali ya Nigeria kuanzisha mchakato wa kuifuta adhabu hiyo ya kifo

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29