Msaidizi wa Katibu Mkuu Feltman azuru Mogadishu kufuatia shambulizi

Kusikiliza /

Mkuu wa masuala ya kisiasa katika Umoja wa Mataifa, Jeffrey Feltman, amefanya ziara nchini Somalia leo kufuatia shambulizi la hivi karibuni kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa, UNSOM, na kusisitiza uungaji mkono wa dhati wa Umoja wa Mataifa kwa serikali ya Somalia na watu wake. Shambulizi la tarehe 19 Juni kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa lilisababisha vifo vya mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa, wakandarasi watatu, walinzi wanne wa kisomali na raia kadhaa. Hii ni ziara ya pili ya Bwana Feltman nchiniSomaliamwaka huu. Bwana Feltman amekutana na rais wa Somalia, Sheikh Hassan Mohamud, mabalozi na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa waliathiriwa na shambulizi la wiki ilopita, na kutoa heshima zake kwa wale waliouawa. Amesema Umoja wa Mataifa hautavunjwa moyo katika kujitolea kuwepo nchini Somaliana kushirikiana nao kwa ajili ya siku zijazo zenye ufanisi kwa nchi yao.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930