Msaada wa Japan kwa ukanda wa Sahel umekuja wakati muafaka: Prodi

Kusikiliza /

Romano Prodi

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Sahel, Romano Prodi ametoa taarifa inayopongeza ahadi ya Japani ya msaada wa thamani ya dola Bilioni Moja kwa ajili ya eneo hilo. Amesema msaada huo ni muhimu kwa eneo hilo linalokabiliwa na changamoto za usalama, maendeleo na uchumi. Bwana Prodi amesema hali tete huko Sahel kama ilivyojidhihirisha hivi katibuni baada ya mashambulio ya kigaidi hukoNigerna maeneo mengine ya mipakani yasiyo na utulivu inaonyesha jinsi ambavyo jumuiya ya kimataifa inapaswa kuchukua hatua za haraka ili kilichofanyikaMalikisijirudie eneo lingine. Mjumbe huyo maalum ametaka jitihada za pamoja za kimataifa za kusaidia eneohilokatika hali inayoeleweka hasa kukidhi mahitaji ya usalama, maendeleo, utawala bora na haki za binadamu na amesema ni matarajio yake kupatikana michango zaidi kutoka nchi mbalimbali duniani.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031