Mgogoro wa Syria udhibitiwe usivuke mpaka: UNHCR

Kusikiliza /

Watoto wa Syria walio ukimbizini Lebanon

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, António Guterres ameanza ziara ya kuadhimisha siku ya wakimbizi duniani kwa kutembelea wakimbizi waSyriawaliokoLebanonpamoja na viongozi wa nchi hiyo inayohudumia maelfu ya wakimbizi waSyria. Katika ziara yake hiyo Bwana Guterres amesisitiza umuhimu mkuu wa kuendelea kuisaidia wakimbizi pamoja na nchi na jumuiya zianzowasaidia na kutahadharisha juu ya  hofu ya mapigano kuenea nchi jirani na kutaka jumuiya ya kimataifa kuungana kuhakikisha vita havienei katika ukanda wa Mashariki ya Kati. Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Lebanon Najib Mikati na Bwana Guterres walitoa wito kwa wahisani na jumuiya ya kimataifa kuchangia kiasi cha dola bilioni 1.7 kinachohitajiwa na Lebanon ambapo serikali peke yake inatoa kiasi cha dola 450 milioni ikiwa ni mchango wake na kuainisha changamoto ambazo nchi hiyo inakabiliana nazo kutokana na kubeba mzigo mkubwa wa wakimbizi ambapo inakadiriwa kuwa hadi mwishoni mwa mwaka huu idadi ya wakimbizi wa Syria walioko Lebanon itafika zaidi ya Milioni Moja. Siku ya wakimbizi duniani huadhimishwa Juni  20 kila mwaka.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031