Mafuriko nchini India, Ban atuma salamu za rambirambi kwa wafiwa

Kusikiliza /

Athari za mafuriko nchini India

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameelezea majonzi yake kutokana na vifo, uharibifu wa makazi na miundombinu nchiniIndiakulikosababishwa na mafuriko kwenye jimbo la Kaskazini la Uttarakhand wiki iliyopita. Msemaji wa Bwana Ban amemkariri Katibu Mkuu akituma rambirambi kwa serikali yaIndia, wafiwa na pole kwa majeruhi na walioathirika kwa namna moja au nyingine na mafuriko hayo. Katibu Mkuu amesifu hatua za haraka zilizochukuliwa na ofisi ya Taifa ya kushughulikia majanga nchiniIndiahuku akisema kuwa Umoja wa mataifa uko tayari kutoa msaada wa dharura wa kuwezesha nchi hiyo kujikwamua kwenye jangahilokadri itakavyohitajika.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031