Kipindupindu chaua watu 257 huko Jamhuri ya Kidemokrasia y a Kongo

Kusikiliza /

Takriban watu 257 waafa kupitia maambikizi ya kipindupindu,DRC

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC yaelezwa kuwa kipindupindu kimesababisha vifo vya watu 257 kwenye jimbo laKatanga kati ya Elfu Kumi na Mmoja waliopata ugonjwa huo tangu mwanzoni mwa mwaka huu.Taarifa hizo ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA kama anavyoripoti Assumpta Massoi.

 (RIPOTI YA ASSUMPTA)

OCHA inasema kuwa idadi kubwa ya vifo viliripotiwa katika mji mkubwa wa Lubumbashi ambao mwezi Mei pekee ulikuwa na wagonjwa Elfu Sita.

Kipindupindu huambukizwa kutokana na kutumia maji yasiyosafina salama pamoja na mazingira machafu.

Kwa mantiki hiyo watoa misaada ya kibinadamu wanajikita katika kutakasa maji na kuendesha kampeni za usafi ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo. Jens Learke ni msemaji wa OCHA.

 (SAUTI YA LEARKE)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2017
T N T K J M P
« ago    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930