Jumla ya watu 93,000 wameuawa kwenye mzozo nchini Syria

Kusikiliza /

Mzozo wa Syria umepelekea maelfu kupoteza maisha,UM

Karibu watu 93,000 wameuwa nchini Syria tangu kuanza kwa mzozo wa kisoasa mwezi Machi mwaka 2011 kwa mujibu wa takwimu mpya zilizochapishwa na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.Zaidi ya asilimia 80 ya wale waliouawa ni wanaume lakini hata hivyo ofisi hiyo ya Umoja wa Mataifa imeripoti kuhusu kuawa kwa zaidi ya watoto 8,200. Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay anasema mauji yanayoendelea Syriani ya kutisha huku watu karibu 5000 wakiuawa kila mwezi tangu mwezi Julai mwaka uliopita.

(SAUTI YA PILLAY)

 Mauji mengi zaidi yanaripotiwa kwenye vitongojii vya mji wa Damascus ambapo kumeripotiwa vifo 17,800. mji waHomsvifo 16,400, Allepo vifo 11,900 na Idlib vifo 10,300.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031