Idadi ya watu duniani inatarajiwa kutimu biloni 9.6 ifikapo mwaka 2050

Kusikiliza /

Idadi ya watu kuongezeka hadi bilioni 9.6 ifikapo mwaka 2050

Idadi ya sasa ya watu wote dunaiani ambayo ni bilioni 7.2 inatarajiwa kuongezeka kwa watu milioni moja zaidi kwa muda wa miaka 12 inayokuja na kufikia watu bilioni 9.6 ifikapo mwaka 2050 kwa mujibu wa ripoti mpya iliyozinduliwa hii leo huku ongezeko hilo likitarajiwa kushuhudiwa kwenye nchi zinazoendelea.Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa idadi ya watu kwenye nchi zilizostawi itabaki bila kubadilika kati ya watu bilioni 1.3 hadi mwaka 2050. Hata hivyo idadi ya watu kwenye nchi 49 maskini zaidi duniani inatarajiwa kuongezeka maradufu kutoka watu milioni 900 mwaka 2013 hadi watu bilioni 1.8 itimiapo mwaka 2050.

Ripoti hiyo pia inasema kuwa hata kama kumeshuhudiwa upungufu kwa watoto wanaozaliwa kwenye mataifa yaliyostawi yakiwemoChina,India,Indonesia,Iran,Brazilna Afrika Kusini idadi ya watu itaongezeka kwenye mataifa yakiwemoNigeria,Niger, Jamhuri ya Kidemokrasi yaCongo,Ethiopia na Uganda.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2015
T N T K J M P
« ago    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
282930