Hali mbaya Syria yaondoa matumaini ya mazungumzo ya amani:

Kusikiliza /

Lakhdar Brahimi

Umoja wa Mataifa, Urusi na Marekani wanakutana mjini Geneva kwa duru ya pili ya mazungumzo ya kufanyika kwa mkutano wa kimataifa kuhusu Syria. Akizungumza kabla ya mkutano wao mwakilishi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Syria Lakhdar Brahimi amesema hali nchini Syria inazidi kuzorota na mipango ya kufanyika kwa mkutano wa kimataifa kuhusu Syria mjini Geneva Julai haionekani kama itawezekana.

Bwana Brahimi amesema majeshi ya serikali na upinzani yanaendelea kushiriki katika uharibifu na mauaji , kuwaongezea wananchi mateso, kutotenda haki na kuondoa kabisa matumaini kwa watu wa Syria.

Amesema mkutano wa Jumanne mjini Geneva utajaribu kutafuta muafaka wa uwezekano wa tarehe za mkutano, nani watakaohudhuria na mfumo utakaofuatwa.

 

(SAUTI YA BRAHIMI)

 

Amerejea ombi lake kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa, kuhusu nchi zinazosaidia pande zinazokinzana katika mgogoro wa Syria ,kuacha kuwapa silaha majeshi ya serikali na waasi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Juni 2017
T N T K J M P
« mei    
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
2627282930