Baraza la Usalama lajadili hali nchini Mali

Kusikiliza /

 

Mali Kaskazini

Kwa mara nyingine tena, hali nchini Mali imekuwa suala la kuangaziwa katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Joshua Mmali amekuwa akiufuatilia mkutano huo.

(TAARIFA YA JOSHUA MMALI)

Mkutano wa leo wa Baraza la Usalama, umehudhuriwa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu kuhusu eneo la Sahel, Romano Prodi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali, Tieman Coulibaly na kuhutubiwa na Mkuu wa Masuala ya ulinzi wa Amani katika Umoja wa Mataifa, Hervez Ladsous, na  Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu Mali, Bwana Albert Koenders, ambaye pia ni mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MINUSMA

Katika hotuba yake, Bwana Koenders amesifu makubaliano ya amani yaliyotiwa saini na makundi yanayozozana nchini Mali, akisema kuwa yanafungua nafasi ya kufanya uchaguzi wa kitaifa, na mazungumzo ya baadaye kuhusu uongozi, haki na sheria, marekebisho ya taasisi za usalama, pamoja na maridhiano.

"Ingawa ni hatua ya kwanza na ya utangulizi, makubaliano haya ni muhimu, siyo tu kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao, bali pia kwayo makundi husika yanatoa ahadi za mazungumzo baada ya uchaguzi. Ili yafanikiwe, mazungumzo hayo yatahitajika kuwa ya kina na jumuishi, na kutatua chanzo cha mizozo ya mara kwa mara nchini Mali."

Koenders amesema pia kwa mujibu wa makubaliano hayo, tume ya kimataifa ya uchunguzi itabuniwa kuchunguza uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu, ukatili wa kingono, mauaji ya kimbari, ulanguzi wa madawa ya kulevya, na ukiukwaji mwingine wa haki za binadamu na sheria ya kimataifa nchini Mali.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031