Baraza la haki za binadamu lataka watu wenye ulemavu wa ngozi (Alibino)walindwe:

Kusikiliza /

Ulemavu wa ngozi picha/UN

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limetoa wito kwa mataifa yote kuchukua hatua zote muhimu kuwalinda watu wenye ulemavu wa ngozi yaani alibino. Alibino ni ulemavu wa kurithi kutokana na gens ambazo zinapunguza utengenezaji chembechembe zionazotengeneza rangi ya ngozi, nywele au macho.Katika azimio lililopitishwa bila kupigiwa kura mjini Geneva Alhamisi baraza limelaani vikali mashambulizi dhidi ya albino na kuzitaka nchi kuhakikisha wanaofanya hivyo wanawajibishwa.Azimio linasema lazima kuwe na uwazi, uharaka na uchunguzi wa kina dhidi ya mashambulio na wahanga na familia zao lazima wawe na fursa ya kupata msaada unaohitajika.

Balozi Baudelaire Ndong Ella wa Gabon, ambaye aliwasilisha azio kwa niaba ya kundi la Afrika , amesema linatoa utangulizi kwa baraza la haki za binadamu kushughulikia suala hilo ambalo linaathiri nchi nyingi.

Balozi Baudelaire Ndong Ella amesema kundi la Afrika linaamini kwamba juhudi za jumuiya ya kimataifa zinahitajika kulinda haki zote za watu wenye ulemavu wa ngozi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031