Ban azungumzia changamoto zinazokabili walinda amani

Kusikiliza /

Walinzi wa amani wanawake kutoka China

Akiwa ziarani nchini China Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amezungumza kwa njia ya video na askari wa nchi  hiyo wanaolinda amani nchini Sudan Kusini alipotembelea kituo cha mafunzo kwa askari hao na kusema miongoni mwa changamoto kubwa za ulinzi wa amani ni kuhakikisha walinda amani wanapatiwa mafunzo ili kukabiliana na vitisho vipya na kufanya kazi katika mazingira magumu. Bwana Ban amesema ujuzi maalum unahitajika katika kutimizahiloili kuwasaidia walinda amani kukabiliana ipasavyo na matukio ya ghafla na kuishukuru serikali yaChinakwa kujitolea kuendesha mafunzo hayo na misaada mingine ya kiufundi ambayo nchi hiyo imekuwa ikitoa katika kutimiza lengo la kulinda amani duniani.

 SAUTI (BAN)

 Kadhalika katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema changamoto nyingine inayowakabili walinda amani ni kusaidia mchakato wa kisiasa katika nchi husika na kuilinda raia katika mazingira hataraishi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031