Ban awapa heko wafanyakazi wa umma

Kusikiliza /

Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Kukabiliana na changamoto za sasa kunahitaji sera za umma za mtazamo wa mbele na mifumo yenye uwazi, na uwajibikaji, na ambayo inazingatia ujumuishaji wa watu maskini zaidi na wanyonge zaidi.Huo ndio ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon kwenye Siku ya Umoja wa Mataifa ya Wafanyakazi wa Umma, ambayo huadhimishwa mnamo Juni 23.

Katibu Mkuu amesema Siku ya Umoja wa Mataifa ya Wafanyakazi wa Umma hutoa fursa kwa nchi kusherehekea mchango wa wafanyakazi wa umma kwa maendeleo ya jamii.

Bwana Ban amesema tuzo za Umoja wa Mataifa za Wafanyakazi wa Umma za mwaka 2013 zinaonyesha jinsi huduma za umma zinavyoweza kutolewa kwa njia timilifu zaidi, bunifu zaidi na kwa usawa.

Ametoa wito kwa wafanyakazi wa umma kote duniani kutenda kazi kwa moyo kama huo ili kuwezesha ujenzi wa siku zijazo jumuishi, zenye ufanisi kwa wote na endelevu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031