Ban awa na mazungumzo na Rais Xi Jinping wa China

Kusikiliza /

 

Ban Ki-moon akutana na rais Xi Jinping, China

Masuala ya uhusiano wa kimataifa, ushirikiano kati ya China na Umoja wa Mataifa hasa katika kukabiliana na changamoto duniani hivi sasa ni miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa wakati wa mazungumzo kati ya Katibu Mkuu Ban Ki-Moon na Rais Xi Jinping wa China huko Beijing, ambako Bwana Ban yuko ziarani. Taarifa ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi.

(RIPOTI YA ASSUMPTA MASSOI)

Ajenda hizo za mazungumzo zilizingatia misingi mikuu mitatu ya majukumu ya Umoja wa Mataifa ambayo ni amani na usalama, maendeleo na haki za binadamu. Mathalani katika amani na usalama Bwana Ban amesifu China kwa mchango wake katika ulinzi wa amani na akashukuru azma ya nchi hiyo kutuma walinzi wake wa amani huko Mali huku akiomba nchi hiyo kuangalia uwezekano wa kutoa mafunzo zaidi kwa walinda amani kutoka nchi zinazoendelea.

Kuhusu Maendeleo amepongeza China kwa uongozi wake thabiti kwenye kuchochea mafanikio ya maendeleo ya Milenia hususan katika kupunguza umaskini na viwango vya vifo vya wajawazito na watoto wachanga.

Halikadhalika wamegusia haki za binadamu na amani katika rasi ya Korea ambapo Bwana Ban ameomba China kuunga mkono jitihada za Umoja wa Mataifa za usaidizi wa kibinadamu huko Jamhuri ya kidemokrsia ya watu wa Korea.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2017
T N T K J M P
« dis    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031