Ban asikitishwa na machafuko Iraq

Kusikiliza /

 

KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema amekuwa akifuatilia kwa masikitiko matukio ya kisiasa na kiusalama yanayoibuka nchini Iraq, yakiwemo kuongezeka kwa hali tete kisiasa na machafuko yalosababisha idadi kubwa ya vifo katika kipindi cha miezi miwili ilopita.

Katika taarifa ilotolewa na msemaji wake, Bwana Ban ametuma risala ya pole kwa waathiriwa na familia zao, na kuitaka serikali ya Iraq kufanya kila iwezalo kuhakikisha walotekeleza maovu hayo wanawajibishwa vilivyo kisheria.

Amesisitizia umuhimu wa kuwepo mazungumzo baina ya makundi ya kisiasa ili kukabiliana na hali tete iliyopo sasa. Amekaribisha juhudi za mazungumzo za hivi karibuni, ukiwemo mkutano ulioandaliwa na Sayyed Ammar Al-Hakim na ziara ya Waziri Mkuu, Nour al-Maliki kwenye jimbo la Kikurdi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031