Ban amteua Abdallah Wafy kama mwakilishi wake maalum DRC

Kusikiliza /

Mwakilishi mpya wa Ban DRC ateuliwa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amemteua Bwana Abdallah Wafy kuwa Mwakilishi wake maalumu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako pia atasimamia idara ya uongozi wa kisheria katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini humo, MONUSCO.Bwana Wafy ambaye amekuwa akihudumu kama Naibu Mwakilishi Maalum kuhusu uongozi wa kisheria katika MONUSCO tangu Septemba 2012 na Mkuu wa idara ya polisi ya MONUSCO, anamrithi Bi Leila Zerrougui wa Algeria, ambaye aliteuliwa kuwa mwakilishi wa Katibu Mkuu kuhusu watoto na vita vya silaha mnamo Agosti 2012.

Bwana Wafy ambaye ni raia wa Niger, alijiunga na MONUSCO mnamo mwaka 2010 kama Kamishna wa Polisi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031